RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Mhadhara - 52:
Kama utafuatilia kwa undani utagundua kuwa biashara nyingi za upangishaji na mauzo ya mali mbalimbali kama vile viwanja, nyumba, mapagala, mashamba, vyumba vya kupanga, mazao, magari, visima vya mafuta, n.k, zinakuwa ngumu kuuzika au kupangishika kwa haraka. Wanaochelewesha biashara ni madalali, na sio wateja.
✓ Kwa mfano:
Unauza nyumba yako kwa Tshs 50mil, lakini dalali uliyempa kazi anamtafuta mteja wa Tshs 100mil ili yeye apate baki la Tshs 50mil (nusu kwa nusu).
Hivyo pasipo wewe kujua dalali wako anaweza kuwakataa wateja ambao watafika na Tshs 60mil, 70mil, 80mil, au 90mil. Kwahiyo biashara yako inakuwa ngumu sana kuuzika au kupangishika kwasababu ya dalali, pengine ulikuwa unataka pesa ya haraka.
✓ Njia za kufanya:
Ukimpa Dalali kazi ya kuuza mali yako (kiwanja, nyumba, pagala, shamba, gari, n.k) ukiona biashara yako inachukua muda mrefu kuuzika, unashauriwa kuwa mjanja sana. Ni ujanja wa kumzunguka dalali wako ili ufanikiwe kuuza mali yako haraka, hakikisha unawapeleleza (unawafahamu) wateja ambao wanashindwana na dalali wako.
Ukiwafahamu wateja walioshindwana na dalali wako watafute ukae nao chemba, itakusaidia kuuza mali yako kwa haraka sana; pia utagundua kuwa biashara yako ilikuwa inakwamishwa na dalali wako. Hivyo mfanye dalali wako kuwa chambo.
Right Marker
Dar es salaam.