Dalali tapeli 0712-571827 anayeshirikiana na polisi

Utamaduni

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
1,279
Reaction score
598
Ndugu wana Bodi heshima kwenu.

Jamani katika kutafuta nyumba za kupanga tuwe makini sana haza maeneo haya ya Sinza, Mwenge, Kijitonyama, Mbezi Beach, Mikocheni etc.

Binafsi na familia yangu tumetapeliwa 4 milioni mwezi huu wa kwanza. Kuna dadali mmoja ambaye ni maarufu kwa jina la DAUDI namba ya simu 0712-571827, huyu anaishi mjini kwa utapeli na ndiye aliyetutapeli sisi. Anatapeli kwa njia ya kukuonyesha nyumba nzuri sana ila cha ajabu anakutajia bei nafuu hadi utamshukuru Mungu kwa kukuwezesha kupata nyumba nzuri hivyo kwa bei nafuu namna hiyo, kwa kweli utasali na kusema hii ni bahati ya Mkenge. Sisi alituonyesha nyumba nyingi kuanzia mwezi wa 12 mwaka jana tulipoanza kutafuta nyumba,, tulimwambia atutafutie nyumba ya laki 4 - hadi 4 na nusu, aliweza kutupeleka nyumba kama 7 (nzuri za laki 3 - 4)bahati mbaya sisi hatukuzipenda hizo nyumba japo zilikuwa nzuri na kwa bei poa sana, hadi alipofanikiwa kutupeleka kwenye nyumba aliyotutapelia ambayo tuliona inatufaa.

Tulipoona nyumba inatufaa, tukamwambia atupeleke kwa mwenye nyumba, ambapo alitupeleka kwa mwenye nyumba FEKI, na tuliandikishana mkataba huu wa kikwetu wa shahidi wawili tukamalizana, ni kama wanakuwa na dawa maana siku zote sisi huwa tunalipa kodi wka cheki, ila this time hatujui nini kimetokea tukaamua kulipa CASH.

Anachofanya, yeye anajua nyumba inayopangishwa, anaenda pale anaongea na mlinz au aliyeachiwa funguo na kuwambia yeye ni dalali, ataleta mteja ila hata kama mteja akirudi baadae peke yake kuthibitisha bei asimtajie bei ya nyumba wala kutoa namba ya mwenye nyumba. Bahati mbaya zaidi tulipotapeliwa na kwenda kufungua kesi polisi, polisi walicheka na kusema huyu mwenye hii namba ni tabia yake, kwanza haitwi Daudi, tulipocheki namba yake kwa tigopesa, tulikuta amejisajili CECILIA MAKOYE.

Ni mvumilivu kukufuatilia, hata ukisema hutaki hii nyumba wala hakulazimishi, na ukimwambia naomba namba ya mwenye nyumba uongee naye ili akupunguzie kodi, anakupa (ya matapeli wenzie) na kwa kuwa wewe huna jinsi ya kuthibitisha huyu ndo mwenye nyumba kweli, unakuwa huna jinsi zaidi ya kumuamini)

hapa tulipo hatuna pa kuanzia kumkamata na ndo tumeumia,

Wanabodi, yaani sijui tunafanyeje ila tuwe makini kupita kiasi, maana huyu dalali mimi nilipewa na mtu ninayemheshimu sana hata nikashinda kumtilia shaka, ajabu hata aliyenipa anashagaa huyu dogo ni tapeli? polisi wanamjua na wanasema anakesi zaidi ya 10 za kutapeli watu hapo kituo cha kawe, ila ndo hivyo

Kama kuna yeyote anayemfahamu mwenye namba hii anisaidie, maana natamani sana nimpate ili niuone uso wake siku atakayoniona, japo najua hela haitorudi tena, ila lazima nimtie japo kilema.
 
Namshukuru Mungu nilibadilisha uamuzi wa kununua binduki. Katika mazingira kama haya hakyamama ningeua mtu!
 
Tatizo watu wakweli huwa hawaamini ila wasanii ndio wanaamika, nakumbuka kuna rafiki yangu aliwahi kuninyima kazi ( siyo udalali) matokeo yake akaangukia kwenye mikono ya wasanii na ameliwa pesa yake na mpaka leo kazi haijafanyika.

Pole sana, huyo huwezi kumuona tena mitaani ni lazima atulie kwenye Air condition ale kipupwe mwezi mzima ndio atoke ndani, 4 millioni kahela kazuri kabisa ni kwa nini apigwe na juwa mitaani?
 
Namshukuru Mungu nilibadilisha uamuzi wa kununua binduki. Katika mazingira kama haya hakyamama ningeua mtu!

Mwingine anajiita Jummaa simu yake ni 0716681716, huyu hushirikiana na Charle wa Mbezi Beach(0755490003 na 0715490003) hawa ni sawa na majambazi. Huuza nyumba na nakala za hati halisi za nyumba wanazo
 
..............Hapo utashangaa Polisi wanakucheka badala ya kutumia intelejensia kuwasaka... wanaendelea kulea maovu..
 
Kinacho shangaza ni pale POLISI wanapocheka na kukwambia jamnaa huyu ni tapeli mzoefu, alafu eti ana kesi zaidi ya kumi kituoni kwao; sasa swali-inakuwaje mtu tapeli anayejulikana kwa vyombo vya DORA anaendelea kupeta barabarani bila ya kubugudhiwa na mtu!! Hii inatoa picha gani kuhusu Taifa letu.
 
Kama police wamesema ndio tabia yake it means alitakiwa kua gerezani ktk maisha yake yote sasa why yuko uraiani?
Police wanahusika!!
 
Pole sana mkuu!...

Siku hizi polisi hakuna msaada basi tu inabidi ukalipoti sababu ni utaratibu!..
 
Pole sana mkuu,kuna watu walishaamua kuwa huo ndiyo mtindo wao wa maisha.
 
Kwa IGP wetu huyu Said Mwema kuna madudu makubwa zaidi ya hayo. Polisi ndio wezi na matapeli kuliko hata matapeli wenyewe. Dawa ni kujichukulia sheria mikononi na kumvunja miguu huyo dalali
 
Ukimuona kijana mwenyewe alivyo smart, huwezi waza utaibiwa.

Nilijaribu kufanya jitihada zangu binafsi kutumia rafiki yangu anafanyakazi tigo kujaribu kuangalia maeneo anayokuwa mara kwa mara, nimegundua huyu anaishi Makondo mana muda wa usiku muda wote simu yake inatumia mnara wa makongo, na mchana anakuwa zaidi maeneo ya Kimara, Ubungo na Mbezi. Tigo wanasema hawawezi kunipa information zaidi za huyu mtu hadi niende na Polisi.

Polisi wameniambia wao hawatotoa polisi hadi nimtafute, nijue alipo, ndipo niwaambie wao waende wakamkamate.

Amini usiamini huyu tapeli bado anapatikana kwenye simu yake kama kawaida, aliifunga siku mbili za kwanza tu, ni kazi yake hii
 
Aisee kuna makauzu zaidi ya Dagaa ili Tapeli nimelipigia simu sasa hivi na linapokea simu bila wasi wasi, mimi sihitaji unipm, Polisi siku hizi wananunulika, kama una vijisenti vya kuwatip Polisi wawili wa Central watakukamatia mtu wako huyu na hutoamini.

Kama uko serious na pesa ulizotapeliwa nikucconnect uende central Police nitakwambia uwaone CID nani na nani, huyu jamaa anakula pingu faster, wameshawahi kukmkamata mtu kwa kumtress huwa anawasiliana na na nani tigo watawaprintia namba zote anazowasiliana nazo, na watakachofanya ni mtu wake wakaribu ndio atakamatwa na ndiye atakayempigia simu yuko wapi na mtaenda kumkamata kama kuku.

Nakuhakikishia pesa yako itarudi huyu atalala central hata wiki wezi wenzake watachangishana pesa kuja Polisi kulipa hizo pesa, wewe unasepa unawaachia kipira wao na Polisi wamalizane wenyewe.
 

Safi sana mkuu,haya sasa Utamaduni kazi imekwisha.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu km unania ya kumkamata nna uhakika unaweza!!! Njia zipo nying sana!,, fanya hii rahisi tumia mtu mwingine ampigie simu amwambie kna uhitaji wa nyumba au chumba then mtangulze huyo jamaa utamkamata! Mm nimempigia cm amepokea nmemwambia nataka nyumba ya kupanga kaniambia tuonane Kijitonyama kesho mchana#
 
Acheni kukurupuka, wezi wa namna hii huwa hawakamatwi hivyo, ukiulizwa namba yake alikupa nani unadhani unaweza kumjibu? nawashauri wote mnaosoma uzi huu msipige tena hiyo namba, huyo huwezi kumkamata bila kumkamata mtu wake wa karibu au ndugu yake au tapeli mwenzake ndio atakuwa chambo cha either kumuita au kumfuata alipo.

Msije mkamu under estimate mtu ambaye amedhurumu millioni 4 na hajakimbia mji na wala hajazima simu wala hajabadilisha namba. JF is home of Great thinkers. Think big.

Utamaduni kama unataka kumpata mwizi wako fuata ushauri niliokupa, huyo yeye si mjinga mpaka leo yuko hewani tena ni jambo la kushukuru kwamba yupo hewani ila hajui kama kuna njia rahisi sana ya kumkamata lakini siyo straight ni lazima akamatwe mtu wanayewasiliana naye mara kwa mara na zile print out za tigo zitaonesha. ukitumia pupa huyo ndio na namba atazima ataanza kutumia namba nyingine.
 
Unajipeleka wewe mwenyewe shimoni hala unamlaumu polisi, kwani ulipopeleka hizo pesa kwa huyo 'rafiki' yako dalali ulimshirikisha polisi? Umeng'atwa sasa unatafuta wa kulaumu eti 'polisi walicheka'. Kuwa makini mkuu, hapa mjini....!
 
Unajipeleka wewe mwenyewe shimoni hala unamlaumu polisi, kwani ulipopeleka hizo pesa kwa huyo 'rafiki' yako dalali ulimshirikisha polisi? Umeng'atwa sasa unatafuta wa kulaumu eti 'polisi walicheka'. Kuwa makini mkuu, hapa mjini....!

duh wee mzima kweli upstairs? Kwani kazi ya polisi ni nini?

Tapeli karipotiwa kwenye vyombo vya dola na polisi haijafanya lolote ili kulinda raia na mali zake kwa maana ya kufanya uchunguzi na kumfikisha huyu mhusika katika vyombo vya sheria, halafu we unakuja na lugha dhihaka kama hii. Yaani ninekuwa na uwezo adhabu ambayo ningekupa ungejuta.....

Kwa mtoa mada tunashukuru sana kwa taarifa na tuzidi kujitahidi kujilinda na utapeli wa aina hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…