Dalali wa Nyumba/Viwanja

Daniel Adrian

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Posts
311
Reaction score
326
Ndugu zangu habari za saa hizi.

Nimetimiza miezi sita sasa sina kazi. Nimetumia taaluma yangu kutafuta kazi lakini jitihada zangu hazizalishi matumaini. Shida ni kwamba sipo peke yangu nina mtoto ananitegemea.

Nimeamua nijiajiri kama dalali wa nyumba na viwanja. Kiukweli sijawahi kufanya hii kazi lakini waswahili wana msemo wao unasema 'njaa ni mwalimu'. Nipo tayari kupokea maelekezo ya mambo yote ninayopaswa kuyajua kabla ya kufanya hii kazi.

Lakini ikiwa pia kuna dalali anahitaji mtu wa kumsaidia au kushirikiana nae nipo tayari ili nipate uzoefu ninaouhitaji.

Kwa sasa nipo Temeke lakini naweza kufanya kazi hii katika wilaya yoyote ile Dar es salaam.

Madalali wazoefu na wabobezi kwenye hii kazi naombeni muongozo wenu (au hata kampani mkipenda) ili nami niijue hii kazi. Namie mkono wangu uende kinywani badala ya kichwani au shavuni.

Natanguliza shukrani kwa wote watakaonisaidia kwa dhati kabisa.
 
Kuna uzi hapa wa Dalali kina jamaa alicomment:- kuna siku dalali akikosa kazi anaweza kimfanyia mkewe udalali. Kila nikionana na dalali hubaki kucheka kwa hio comments[emoji23][emoji23].


Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 

Usiweke tamaa mbele tu, watu siku hizi hawawapendi sababu ya tamaa zenu za kijingajinga mara mpewe kodi ya mwezi, katika viwanja mnakula hata mara 2 ya muuzaji

Ushauri: tengeneza group za whatsapp weka watu jitofautishe na wenzio
 
Daniel Adrian
kazi ya udalali sio sawa na kazi ya ofisini

dont give it 100% assurance kwamba ndio kazi ya kukuweka mjini, No!

udalali unaweza kaa hata miezi mitatu huna tenda, especially kwa beginners kama wewe!

mimi wakati naanza hii kazi, nilianzia kuuza simu, hii ndio the fastest way ya kukupa hela!

Otherwise sisi madalali tunaroga sana,
Kuna wateja wanatuzungusha mnooo, so bila kuroga sana hatufanyi biashara!

kuna mtu ananunua nyumba baadae anajiuliza nimenunuaje hapaπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ€£πŸ€£
 
Usiweke tamaa mbele tu, watu siku hizi hawawapendi sababu ya tamaa zenu za kijingajinga mara mpewe kodi ya mwezi, katika viwanja mnakula hata mara 2 ya muuzaji

Ushauri: tengeneza group za whatsapp weka watu jitofautishe na wenzio
Asante sana kwa ushauri wako.

Kila dalali ana utaratibu wake wa malipo. Si kila dalali anataka kodi ya mwezi mmoja.
 
Kuroga ukimaanisha masuala ya kishirikina ?. Mimi siamini katika katika mambo ya kishirikina.

Asante kwa ushauri wako kuhusu isiwe kazi ya kuniweka mjini 100%
 
mungu anawaonaa.... ila dalali kwa nini leo unaweza fanya dili ukapata pesa ila kesho yake ukaja huna ata mia ? kwa nini
 
mungu anawaonaa.... ila dalali kwa nini leo unaweza fanya dili ukapata pesa ila kesho yake ukaja huna ata mia ? kwa nini
pesa ya dalali ni kama pesa ya watu wa migodini au watu wa tour guide..

Easy come, easy go!
 
Reactions: Lee
nimekuelewaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…