#COVID19 Dalili mpya za COVID-19 za kuzingatia

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124


Licha ya dalili za awali zinazotambulika tangu wimbi la kwanza, pia kuna dalili nyingine zinazogunduliwa na madaktari hivi karibuni, ambazo zinahitaji uangalifu.

Madaktari nchini India wanaamini kuwa baadhi ya dalili zinazidi kuongezeka katika visa vilivyoripotiwa tangu mwezi uliopita.

Vidonda kwenye mdomo na ulimi
Madaktari wanabainisha kuongezeka kwa idadi ya visa vinavyojitokeza na dalili kama vidonda kwenye mdomo na ulimi ambavyo huambatana na dalili nyingine kama homa , kikohozi na uchovu.

Uvimbe kwenye ngozi na vidole
Kuna visa mbalimbali ulimwenguni kote vya wagonjwa wa Corona kuwa na uvimbe kwenye ngozi na vidole vya mikono.

Harara na vinundu kwenye ngozi
Wataalam wa Afya wanabainisha kuwa harara inayoweza kudumu kwa masaa kadhaa ni moja ya dalili ya Corona katika siku za mwanzo, pia huweza kusalia hata baada ya kupona Corona
 
Duuh tunapoelekea mtu atakayepata maambukizi ya corona atakuwa anatisha sana, Mungu atuepushe na hili jinamizi
 
Epukaneni na mikusanyiko, maharusini, disco, cinema n.k ndugu zanguni. lakini hamusikii mpaka mkuu awachape makofi kama kenya wanavyofanya dio muache.
 
Corona tunaishi nayo
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…