geranteeh
JF-Expert Member
- May 21, 2015
- 268
- 646
Usukani ni kitu ambacho hata mtu ambaye hajui gari anafahamu, ni kitu ambacho hata watoto wadogo wanakijua lakini ukweli ni kwamba watu wengi sana ikiwemo madereva ambao wana leseni na uzoefu hawajui kiundani mfumo mzima wa usukani. Kutofahamu kitu kiundani pia humaanisha hata linapotokea tatizo kwenye mfumo ni ngumu pia kuelewa hali inayopelekea shida kuwa kubwa zaidi na kuleta madhara au ukatumia gharama zaidi.
Teknolojia hubadilika miaka na miaka na vivyo hivyo kwenye teknolojia ya usukani, gari za miaka hiyo ilikua unatumia nguvu zaidi katika kukunja usukani tofauti na gari za kisasa kumbuka teknolojia hufanya mambo kuwa mepesi zaidi kwani kwa gari za kisasa unaweza kunja usukani bila kutumia nguvu zaidi yani hata mtoto mdogo anaweza kunja usukani vema zaidi bila hata shida yoyote tofauti na gari za zamani.
Katika kesi ya kufeli kwa mfumo wa usukani uendeshaji wa gari huwa mgumu sana. Mimi binafsi yalishawahi nikuta na kivumbi nilikiona na kama ni legelege unaweza sababisha ajali na kumbuka mda wote usukani huwa ni mgumu yani afadhali yako ni pale gari inapokuwa kwenye mwendo kidogo ugumu hupungua sasa fikiria upo kwenye foleni alaf unataka utoke huku uingie huku sehem inayohitaji uharaka hakika utasababisha ajali.
Kama ilivyo matatizo mengi ya gari huwa yanakuja na dalili na pindi unapopuuzia dalili basi hakika shida itakukumba, Hapa chini nitaelezea dalili ambazo ukiziona jua kwamba mfumo wa usukani wa gari yako una shida na unahitaji kuangaliwa na fundi ila kumbuka kuna aina mbili za huu mfumo wa (Power steering) kuna za umeme na kuna za kawaida na pia hizi za umeme ni ngumu sana kurekebisha hivyo pindi zinapoharibika unatibu kwa kubadilisha mfumo mzima tofauti na za kawaida kuna namna zikiharibika mafundi wetu wanaweza wakazirekebisha hebu tushuke kwenye dalili za kufeli kwa mfumo wa usukani.
1. MLIO PINDI UNAPOKATA KONA AU KWENDA MWENDO MDOGO
Kumbuka katika gari yako kama nilivyowahi elezea mlio wowote ambao si wa kawaida hautakiwi ila endapo unaendesha gari na ukasikia mlio pindi unapokunja kona au kwenda taratibu wazungu wana majina ya milio ila sisi mlio ni mlio wneyewe wanaita Squealing na Whining noises. Inaweza kuwa ni shida ya pampu ya Steering inakaribia kufeli au pia mlio wa ajabu pindi unapowasha gari yako huweza pia kuwa ni shida ya pampu hivyo basi unatakiwa kuchukua hatua.
2. MTETEMEKO KATIKA USUKANI WAKO
Unapoendesha gari yako au gari ikiwa Idle alafu usukani ukiwa hautulii unatetema kama vile simu ikiwa kwenye vibration basi jua kuna shida kwenye mfumo wa usukani na shida hii au kutetema huku huzidi pale unapowasha AC na hii dalili hutokea ghafla bila kuwa na hodi na mara nyingi dalili hii husababisha au hutokana na kulegea ama kuharibika kwa mkanda endeshi (Drive Belt) hivyo basi unahitajika kuubadili. Kumbuka drive belt inahitajika kuwa sawa ili kuifanya pump ya steering kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.
3. UGUMU PINDI UNAPOKUNJA KONA
Dalili nyingine ya shida katika mfumo wa usukani ni kupata ugumu pindi unapokunja kona na watu wengi hustuka wanapoona dalili hii zaidi.Shida hii sababu kuu huwa ni kupungua kwa kiwango cha kimiminika kwenye mfumo wa usukani yani (Power steering Fluid) lakini pia inawezekana ikawa inasababishwa na kupungua kwa upepo kwenye tairi ya gari yako au kutokana na ishu za wheel alignment hivyo basi endapo ikikutokea angalia sababu hizo tatu.
4. KUPUNGUA KWA MARA KWA MARA KWA KIWANGO CHA KIMIMINIKA CHA MFUMO WA USUKANI.
Inawezekana ukawa ni mtu wa kufuatilia sana viwango vya vimiminika kwenye gari yako yani kwanzia oil ya injini, Kimiminika cha Gearbox na kimiminika cha mfumo wa breki lakini kwenye kimiminika cha mfumo wa usukani unakuta kila baada ya muda kinakuwa kinapungua pamoja na kwamba unakuwa unaongeza kila baada ya muda fulani, Hakika hii ni dalili kwamba kuna sehemu kimiminika hiki kinavuja hivyo basi ni bora ukafuatilia mfumo kabla gari haijaanza kupoteza kwa kiwango kikubwa ikakusababishia kuua kabisa mfumo mzima.
NINI CHA KUFANYA ENDAPO MFUMO UMEHARIBIKA IKIWA GARI IPO KWENYE MWENDO?
Kumbuka gari ni chombo cha usafiri ambacho kimetengenezwa na binadamu hivyo kasoro hutokea mda wowote sasa iwapo itakutokea ukiwa kwenye mwendo maana usukani huwa mgumu ghafla hivyo cha kwanza hutakiwi kupaniki kwani adui wa kwanza kwenye udereva ni kupaniki kwani akili inakuwa haitendi kazi ipasavyo yani kichwa kinakuwa hakijatulia na unaweza ukachukua maamuzi yatakayo kugharimu, Punguza mwendo wa gari yako taratibu usifunge breki za ghafla kwani utasababisha madhara zaidi kwa waliomo ndani ya chombo na watumiaji wengine wa barabara alafu washa Hazard Light ili watumiaji wengine wapate kujua kwamba una shida kwenye chombo chako.
Tafuta sehemu salama uegeshe chombo chako na baada ya kuegesha zima gari yako. Baada ya apo kazi inayofata ni kukagua mfumo mzima wa Usukani kwanzia Mkanda endeshi (Drive Belt), Kiwango cha kimiminika kama kiko sawia na hoses mbalimbali za mfumo hakika hilo litakupa picha kamili ya shida ipo wapi na ukaweza kuwasiliana na fundi wako na kama kuna kifaa chochote kinahitajika unaweza nitafuta, Kumbuka Mfumo wa usukani unaweza ukarekebishika ama ukahitaji kubadilisha mfumo mzima hasa hizi za umeme.
Imeandikwa na Hamis Mgaya
0655513132