Dalili ya Kufa Penzi

Dalili ya Kufa Penzi

Power G

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Posts
3,884
Reaction score
1,198
Nina uhakika wengi wetu (kama siyo wote) katika maisha, tulishapenda, kupendwa, kuacha na kuachwa vile vile. Kwa hiyo katika mahusiano tunajua wazi kwamba penzi huzaliwa, hustawi na wakati ukifika hujifia. Lakini kabla ya penzi kufa ni viashiria vipi au dalili gani ambazo zikionekana, mhusika ataziona kwa mwenzake kuashiria kwamba penzi lake sasa liko ICU? Nadhani uzoefu wenu katika mahusiano utasaidia kujibu hili swali ili mhusika ajue mapema dalili aweze kutafuta dawa ya kuzuia penzi lake kufa.
 
Lakini kabla ya penzi kufa ni viashiria vipi au dalili gani ambazo zikionekana, mhusika ataziona kwa mwenzake kuashiria kwamba penzi lake sasa liko ICU? .

Ukianza ku-compare mpenzi wako na mtu mwingine..hujue hakuna kitu hapo..
 
Ukianza kukasirikia mwenzio na kuongea kwa hasira kwa 7bu ya vitu vidogoyo ambavyo mwanzon mlikuwa mkieleweshana na kuyamaliza bila hasira wala mzozo.
 
ukitaka ng'ong'o af mwenzio anaanza vijisababu mara nimechoka mara sijisikii,aaah hapo huna chako
 
Akienda ht kuoga yupo na simu au anacha kazima....WIZI MTUPU hapo!
 
Unaandika masage nzuri na ndefu kidogo mwenzako anajibu kwa ufupi either yes or no ama poa...hapo ujue umeumia
 
Duh...! ngoja nikaorodheshe will be back
 
dharau,kejeli,mawasiliano kuanza kuyoyoma taratiiibu,ukikaa naye mara mi namuawai mama cjui mamdogo kaniita so mi naondoka,ukimuita yy kukupa sababu tuonane kesho leo cwez,kuanza kukubebesha mamizigo hata hayakuusu ili uchoke umuache,akianza kutokukujali hata kama unatabu yy hakuonei huruma anaona ni kawaida tu,kuanza kukuambia mbona mm hunifanyii kama flani anavofanyiwa na mpz wake,
.......................hahaaaaaaaaaaaaaaa hapo sasa MULIKA MWIZI
 
Mnazifahamu vyema!nadhani wote mna experience ya KUFIWA na mapenzi.
 
Ukiona hizo dalili ni bora ujiweke pembeni uepushe msongamano, maana !!!!
 
Back
Top Bottom