Dalili ya mvua ni mawingu, Ni vyema TANESCO watuwekee mkeka wa mgao wa umeme tuzoee kabisa!

Dalili ya mvua ni mawingu, Ni vyema TANESCO watuwekee mkeka wa mgao wa umeme tuzoee kabisa!

mkulimamiwa

Member
Joined
Mar 4, 2025
Posts
39
Reaction score
36
Sifahamu shida ni nini

Vimikatiko vya umeme visivyoeleweka vimekuwa vingi kiasi cha kujiuliza maswali iwapo tayari Tanesco wameshaanza kutoa dozi ya mgao wa umeme

Wakati matamko ya viongozi mbalimbali yakitolewa ya kutokuwepo mgao wala usumbufu wowote wa umeme hata kwa misimu mitatu ya ukame nchini,

Hali inayojitokeza sasa ni ya sintofahamu na tunaanza kujiuliza Je, tuamini lipi kati ya hayo mawili, tuwaamini Tanesco kwamba, nchi inahaki ya kuwa na mikayoko ya umeme mara kwa mara kwa sababu pengine ya ukweli walionao wao, au tuendelee kuamini matamko ya viongozi wetu?


Tanesco ndio wanao kaa na jiko, ndio wapishi, wanajua fika kile kilichoko kwenye vyanzo vyetu vya umeme, au tu Tanesco wanataka kuwachonganisha viongozi wetu na wananchi waliowapa dhamana ya kuongoza nchi?

Watanzania ni watu waliozoea kuongopewa na siyo kuambiwa ukweli, ukisikiliza sababu nyingi za Tanesco za kwa nini umeme unakatika, wao watasema, wapi kwenye matengenezo sjui ya nguzo na nyaya...

Kama sababu ni hiyo, Je, ni lini watakamilisha matengenezo na kuacha umeme ukae hata mwaka bila kukatika?

Ni lini tutafikia huko? Mawazo yangu, huu ulishakuwa kama mchezo tu ilihali ukweli wanaujua, na ndiyo maana kuna wakati akili za watanzania, mambo haya yanapokuwa ya kujirudia rudia sana, huwa tunaamini ni hali za mgao tu wa umeme wala hakuna lingine

Ni vyema tuwe tu wakweli, mnachosha sana Tanesco
 
Back
Top Bottom