dalili ya saba unajidanganya.wanaochangia CHADEMA NI WACHAGA TU, kwani wana maslahi na hicho chama chenu cha kikabila. dalili ya nane nayo ni uwendawazimu kuitilia maanani kwani wengi wanaopost comment zao humu ni washabiki wa CHADEMA ambao kuna ushahidi kuwa si wapiga kura( kumbuka hata Mrema alibebwa kama jeneza lakini aliangukia pua. CCM imewekeza kwa wazalendo wa hali ya chini ambao hawajui hata computer ina umbo gani na for sure wao ndio wapiga kura.
panua miguu na uwe tayari kufanyiwa tohata(kutahiriwa) kwa mara nyingine
Mkuu ili hoja yako ieleweke siyo lazima utumie lugha kali kama ilivyo kwenye sentensi yako ya mwisho.
Hapo kwenye uwekezaji ndipo ambapo ninaomba ufafanue, mmewekeza nini? The only way ya kuwekeza kwa watu wa chini/vijijini ni kwa kuboresha bei za mazao yao, hapo ni total failure. Kila kona bei ya mazao ni mbaya kuliko. Kuanzia kahawa, tumbaku, pamba, mpaka mahindi. Bado miundombinu ya vijijini ni zero, maji zero, afya zero, elimu ndo usiseme kabisaaaa. Hebu niambie huo uwekezaji unaousema ni upi?
Usiwatukane wakazi wa vijijini, sema ukweli kwamba mnatumia ujinga wao au kutojua kwao haki zao na ndio maana mnapata kura. Zikitokea NGOs kama HakiElimu zikaanza kuelimisha jamii serikali inakuja juu. Hata Zimbabwe ilikuwa hivyo hivyo, ushindi wa Mugabe ulikuwa unatoka vijijini, iko siku waliamka na kujua haki zao. Hata Tanzania ya leo mwamko upo, taratibu mtaondoka tu, maana wananchi wanaamka na kuelewa haki zao na kujua adui yao wa kweli ni nani.
Mwaka 2005 mlipeta kilaini, mwaka huu hali ni ngumu ndio maana mmeanza kutoa hata ahadi ambazo hazitekelezeki na kusema uongo juu. Mojawapo ya mambo ambayo mmesema uongo ni pamoja na JK kusema amepandisha mishahara halafu waziri wake anasema HAPANA, wote wako ndani ya serikali moja. Mnaahidi kugawia watu ardhi na kumbe mlishauza kwa wawekezaji, Kigamboni wamewabana mseme agenda yenu, JK kaingia mitini anasema ni jukumu la diwani, yaani maamuzi lifanye baraza la mawaziri, halafu umsukumie diwani? Hata aibu hana! Mmewadanganya wakulima wa mahindi wa Mby kwamba wakauze mahindi yao SGR na kumbe hakuna hela. Mamlaka ya Korosho baada ya kuona cheche za Prof Lipumba juzi wamejifanya kutangaza kufungua msimu wa kununua korosho, ajabu ni kwamba hawana hata senti wanategemewa wakanunue mali kauli!
Huo ndio uwekezaji wenu kwa kutumia ujinga wa watu wa chini kabisa ambao umewaelezea vyema kabisa kwamba hawajui hata computer, sema kabisa kwamba hawajui hata kusoma, maana ujinga wao ndio mtaji wenu! So sad ... na unasema kwa ujasiri kabisa kwamba mmewekeza kwenye ujinga wao!