Dalili za kifua kikuu

Dalili za kifua kikuu

Chuck j

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
2,366
Reaction score
828
Naomba kujua dalili za mwanzo kabisa za kifua kikuu,,
 
1. Kikohozi kikavu ambacho hakisikii antibiotic mfululizo kwa zaidi ya wiki mbili.
2. Kutoka jasho usiku, ambalo linalowanisha hadi nguo ulizolalia.
3. Homa hasa usiku
4. Kukonda
5. Ukipima makohozi yataonyeha uwepo wa bacteria ingawa si wakati wote.
Wakti mwingine unaweza kukohoa damu.
 
Kifua Kikuu - TB

TB au Kifua Kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na viini viitavyo ‘tubercle bacilli’.
Wengi wetu tuna viini vya TB mapafuni mwetu lakini hii sikumaanisha kwamba tutauguza huu ugonjwa. TB hushika wale ambao wana ukosefu wa kinga mwilini unao sababishwa na kutokula chakula kizuri, matumizi ya madawa ya kulevya au wanaouguza magonjwa mengine.

TB ya mapafu ndio imeenea zaidi. Hata hivyo, viini vya TB vinaweza kusafirishwa kutoka mapafuni kupitia kwa damu hadi sehemu zingine za mwili na kusababisha hivyo viungo viathiriwe na TB.

Viini vya TB hupatikana kwa mate ya muuguzi. Wakati mgonjwa anakohoa, kupiga chafya au kutema mate kiholela, viini vya TB husambazwa kwa hewa. Mwenye afya akiipumuwa hewa hiyo anaambukizwa na mapafu yake inaanza kuwa na vijidonda.

Dalili za TB


  • Kikihozi kisichoisha
  • Uchovu na kuishiwa kwa nguvu mwilini
  • Kupoteza uzito
  • Kupoteza hamu ya kula
  • Kutokwa na jasho hata wakati kuna baridi
  • Maumivu ndani ya kifua
  • Kuishiwa na pumzi
  • Mate yaliyo na damu au kukohoa damu
 
Back
Top Bottom