Dalili za uchizi

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Tunaposema fulani ni chizi au mwendawazimu tunamaanisha kuwa hatumii ipasavyo akili zake.
Kila mtu ana akili isipokuwa maiti ila utofauti unakuja kwenye matumizi ya akili.
Zifuatazo ni dalili za uchizi;
1. Kukataa mimba huku unajua ni yako.
2. Kujenga mbali na kazini kwako huku unajua kabisa kuwa huna usafiri .
3. Kutoa mimba
4. Kuvaa kondomu wakati wa kufanya mapenzi.
5.Kusuka nywele kisha unazichambua kama mchicha.
6. Kuvaa suruali iliyochanwa kwenye magoti au mapaja.
7.Mwanaume kuvaa hereni
8. Mwanaume kusuka.
9.Kujipiga picha kwenye majengo ya fahari kisha kurusha mitandaoni huku unalala kwenye kibanda umiza.
10. Kupost picha kila unaponunua nguo mpya.
Nitakuja kuendeleza mkeka
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]utasutwa
 
1. Namba 1 utajuaje mimba ni yako kwamba ukitia mimba inakuhakikishia hii ni y'ako.
 
Jamaa hataki tuvae kondomu halafu tusikatae mimba na dada zetu wasitoe mimba Sasa si bora tuvae ili wasipate kabisa na tusikatae hizo mimba, anyway sasa tusipovaa UKIMWI unajua utatuangalia kwa sura gani ndugu..?

Msinihoji kwanini sijaona mengine issue ni ajenda tu,huwezi kuwa manager wa benki halafu ubase kuzungumzia majimaji war..😎
 
 

Mtoa uzi ni chizi mmoja ambaye una stress za watu zinazokuchanganya na kwa ufupi una gubu la life za watu
 
Kujenga mbali na kazini kwako huenda ni busara, sio uchizi. Nauli unayotumia kwa mwezi ni ndogo ukilinganisha na kodi ya nyumba. Nyumba yako ni mahali pa usalama wewe na familia yako. Unaonaje nikaishi mjini kwa kupanga na kununua gari ndogo ya usafiri hata mahali pa kupaki ni shida? Huu ndio uchizi wa daraja la kwanza.
 

Kupitia uzi huu umejionesha kuwa nawe hizi dalili zaweza kuwa zinakuhusu.

1. Kujenga mbali inaweza kusababishwa na kipato kwamba mtu kashindwa kumudu gharama za viwanja maeneo ya karibu
2. Kuvaa kondomu sio tatizo kwani hata wana ndoa wanaweza vaa ili kuhakikisha mwanamke habebi mimba. Inawezekana hawataki mtoto na nyege zimepanda.
3. Kuweka bleach kwenye nywele ni fasheni tu kwa wengine. Wewe kama haikufai waachie wengine na ni uchizi kutaka kila mmoja anyoe kama wewe
4. Kuvaa suruali iliyochanwa pia ni fasheni kwa wengine na chizi pekee atataka wote wavae conventional jeans au suruali
5. Wanaume kuvaa hereni pia ni asili ya makabila mengi tu hata hapa kwetu na kwa wengine ni fasheni tu na ukikaa vibaya watapita hata na mkeo kwani haina maana yoyote kwenye their sexual orientation.
6. Kusema wanaume wanaosuka ni dalili ya uchizi pia mkuu.

Discalaimer

Nimetoa mtazamo wangu tu mkuu. Ila hayo yote ya kusuka, kuvaa nguo imechanwa, kuvaa hereni mie situmii ila naona ni dalili za uchizi kuanza kufuatilia maisha ya watu wakati yangu tu yananitoa jasho

Karibu
 
Duh kweli una Moyo Sana kumjibu kwa kirefu namna hi?
 
Kazini kwako kwa maana ya kuwa wewe ndo mmliki wa hiyo ofisi au ni mwajiriwa, ambaue wakati wowote kibarua kinaweza kuota nyasi!???
 
Kuna point zingine hapo zinafurahisha sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…