achengula
JF-Expert Member
- Jul 30, 2009
- 369
- 62
Ugonjwa huu unawasumbua sana wafugaji wa kuku (na jamii yake) na mifugo mingine. Ziko aina kuu mbili za ugonjwa huu kwa kuku kutegemeana na eneo ambalo linashambuliwa kwenye utumbo. Coccidia wanaweza kushambulia kwenye utumbo mwembamba (intestinal coccidiosis) au sikamu/tawi butu (caecal coccidiosis) na hata madhara yake yakajitokeza maeneo hayo tena kwa kuku wa umri tofauti. Coccidiosis ya sikamu/tawi butu (caecum) inawapata kuku wadogo wa hadi umri wa miezi 6 na wanasababishwa na coccidia anayeitwa Eimeria tenella. Coccidiosisi ya utumbo mwembamba inawapata kuku wakubwa na inasababishwa na aina nyingi za Eimeria zikishambulia maeneo tofauti tofauti ya utumbo mwembamba. Wapo wanaoshambulia mwanzoni mwa utumbo mwembamba (E.acevulina), katikati (E.necatrix) na mwishoni mwa utumbo mwembamba (E.brunetti).
Dalili za coccidiosis kwa kuku na jamii yake soma hapa SEKTA YA MIFUGO TANZANIA
Dalili za coccidiosis kwa kuku na jamii yake soma hapa SEKTA YA MIFUGO TANZANIA