Mkuu Shana Boy DALILI NA ISHARA ZA UJAUZITO
Dalili za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, ingawa kuchelewa au kukosa hedhi ni dalili moja muhimu sana.
Ni muhimu kuzitambua na kuzifahamu dalili hizi kwa sababu zinaweza kusaidia kuelezea au kutofautisha matatizo mengine mbali ya ujauzito.
Hebu sasa tuangalie dalili na ishara za Ujauzito:
Kutokwa damu kidogo ukeni wakati kiumbe kikipandikizwa kwenye mfuko wa uzazi, ingawa siyo wanawake wote hupatwa na dalili hii
Kukosa hedhi, hii ni moja ya dalili kubwa za ujauzito
Maumivu ya matiti na kuvimba matiti (huweza kutokea kati ya wiki ya 1 hadi ya 2)
Uchovu, wanawake wengi hujihisi uchovu na hali ya kutopenda kufanya lolote.
Kupoteza ladha au kuhisi ladha ya chuma mdomoni
Kuongezeka kwa hisia ya harufu, kipindi cha ujauzito wanawake wengi huongezeka hisia ya harufu
Kichefuchefu na kutapika
Maumivu ya kichwa
Kizunguzungu
Kukojoa mara kwa mara (hasa kati ya wiki 6-8)
Kubadilika rangi kwa ngozi inayozunguka chuchu kuwa nyeusi
Kutamani baadhi ya vyakula na kuchukia vingine
Kupanuka kwa mfuko wa uzazi
Tumbo kujaa au kuvimbiwa
Kununa na kukasirika haraka
Kiungulila au kupata choo kigumu
Kolostramu kuanza kutoka kwenye matiti
Kuongezeka uzito
Kuweza kupapasa mtoto (palpation of the baby )
Kulainika na kuvimba kwa shingo ya uzazi (Hegars sign) - kuanzia wiki ya 6
Shingo ya uzazi kubadilika rangi kuwa ya samawati kutokana na msongamano wa damu katika mishipa ya vena. Ishara hii huitwa pia Chadwick's sign
Dalili nyingine ni pamoja na
Mstari wima mweusi hutokea tumboni kuanzia chini ya kitovu (linea nigra )
Mama kuhisi mtoto akicheza (kuanzia wiki ya 20)
Maumivu ya mgongo hasa mimba ikishakuwa kubwa.
Kipimo cha mimba kuwa chanya (positive).
Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto
Mtoto kuonekana kwenye kipimo cha ultrasound
Katika makala itakayofuata tutaangalia vipimo muhimu vya kudhibitisha uwepo wa ujauzito. Usikose... Dalili na Ishara za Ujauzito
Last edited by a moderator: Jan 4, 2016