Del cymon
New Member
- Apr 23, 2019
- 1
- 2
Wakati serikali inajitahidi kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana kwa kutoa mikopo nafuu kwa vijana kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza biashara na shughuli mbalimbali za ujasiriamali, jitihada hizo zinazimwa na watendaji wa ngazi za chini hasa katika ngazi ya kata ambapo kumekuwa na upotoshaji wa makusudi kabisa lengo kuu ni kujipatia pesa kutoka kwa waombaji.
Ukilichukulia kwa haraka inaonekana ni utaratibu na upo kisheria na huenda ukadhani unasaidiwa. Juzi mimi binafsi nilifikiria kuanza mchakato wa kusajili kikundi walau ninufaike nami nijikwamue huenda nikafika mahali na wanakikundi wenzangu.
Nilianza vizuri kabisa ngazi ya mtaa hakukuwa na shida yoyote. Kizaazaa knaanza katika hatua ya kati ambapo nilitakiwa kuchukua barua ya utambulisho kutoka kwa afisa maendeleo au mtendaj wa kata ya Engutoto jijini Arusha.
Picha linaanza ile nafika ofisini baada ya salamu naeleza shida yangu hata kabla sijamaliza naambiwa hilo ni jukumu la afisa maendeleo ambaye yuko safarini. Lakini nikaambiwa nisijali kwa kuwa huduma nitaipata kwani ameacha maelekezo kwenye stationery hapo jirani na ofisi ya kata hivyo nitahudumiwa vizuri kwani wao wanajua kila kitu.
Changamoto haikuwa kuhudumiwa na stationery kila ninachohitaji kwani nilicho hitaji ni kupata huduma. Kilichnishangaza ni gharama ya kuprocess mchakato mzima ambayo ni TSH 100,000 ambapo elfu hamsini 50,000 itakuwa malipo ya kufanya maombi ya usajili kwenye mfumo, na elfu hamsini nyingine itakuwa kama ada ya maombi ambayo itatumwa halmashauri ilikusudi mfumo ufunguke na kuwa nitapewa control namba.
Kuonyesha kuwa hawana haja na pesa yangu ila wanahitaji kunisaidia tu, nikaambiwa kama naona ni gharama basi nijaribu mwenyewe kuomba kwenye mfumo ila nikasisitiziwa kuwa wao(stationery) ndio wanajua vizuri format inayotakiwa.
Kimsingi mimi pale nilienda kuhitaji barua moja tu ya utambulisho hivyo nikawaambia watu wa stationery kuwa nahitaji barua pekee ili niendelee na usajili ninavyojua mimi.
cha kushangaza ni jibu nililopewa kwamba hawafanyi vitu nusu nusu kwamba ili kusudi wanisaidie inanididi nilipe hiyo laki moja au niitafute hiyo barua ya mtendaji ninakojua mimi.
Katika ufuatiliaji wangu nikaja kugundua kuwa hata ada ya maombi tu hakuna kwani kujisajili ni BURE kabisa ni mtu, bando lake na gharama kidogo za kuscani documents zinazohitajika, deal done.
Lakini barua moja tu ambayo ni ya muhimu imekataliwa, imekuwa chanzo cha kitega uchumi cha sfisa maendeleo mmoja na business partner wake ambao wamnafanya vijana tuonekane tuko nyuma katika kuitikia fursa.
Imagine sina ajira rasmi, kula ni asante baba unashukuru jua likisha tua, ukiamka unawaza siku inaishaje, kodi tu ya chumba ni shughuli kuilipa unafanya kumpiga fix mwenye nyumba na kumpooza na kiasi kidogo kidogo kumuaminisha kuwa una nia ya dhati kabisa ya kulipa kodi yake ni vile tu pesa hakuna, halafu unasikia fursa tena kutoka kwa serikali unabaniwa mrija kutoa kiasi ambacho kwa hali halisi ni kikubwa sana kwa kijana kama mimi mgaa gaa na kupwa.
"Infact ni kama elfu ishirini tu kwa kila mwanakikundi" mhusika wa stationery aliniambia hivyo. Ukimsikiliza kwel unaingia kingi na unagundua ni rahisi tu kuilipa lakini tujiulize tu, ni vijana wangapi wana huo uwezo? Na hata kama wanao kwanini anyonywe mnyonge, mamlaka ya kujitungia utaratibu wanapata wapi? Au pengine mimi ndio mjinga sijui chochote🤷♂️! Kama kuna mtu anauhakika kuna malipo anisaidie nisije kuwa na hukumu bure lakini bado najiuliza
1. Kwanini aache maelekezo na kukabidhi kazi nje ya ofisi au utaratibu wa siku hizi unasemaje wadau?
2. Kama sio mbinu ya upigaji ni kwanini nisipewe barua niende kuyatavanga mwenyewe?
3. Na kama wana huruma kiasi hicho kwa nini wasinipe huduma nikalipie kidogo kidogo?
Anyways sijui kwa nini tukijikuta sisi ndio final say au karibia na final say kuhusu jambo fulani tunajikuta miungu watu sijui hatanimalizie vipi kama kuna mtu ana uzoefu mzuri na hizi taratibu nisaidieni kujua kwa kina wadau