Dalili zifuatazo zinaonyesha utakapoolewa utateswa au kuteseka

Dalili zifuatazo zinaonyesha utakapoolewa utateswa au kuteseka

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
DALILI ZINAZOONYESHA UKIOLEWA UTATESEKA AU KUTESWA SANA

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kwa Wanawake wengi Ndoa ni Kaburi, Ndoa ni Gereza la Guantanamo. Nikiwa sitaki Leo kuleta Fujo Sana na kugombana na Mtu yeyote naomba niandike kifupi Sana.

Dalili zifuatazo zinaonyesha utakapoolewa utateseka na kuteswa Sana;

1. Huna Kazi na unamtegemea Mwanaume Asilimia 100%
Hakuna ubishi wowote kuwa usipokuwa na Kazi na Ukawa unamtegemea Mume wako Kwa Asilimia Mia Moja Hakika utateseka Sana. Lazima uteswe.

Wanawake wengi unaosikia wanateswa Hawana Kazi ya kufanya zaidi ya kuwa Mama wa Nyumbani tuu.

Watu watakaokutesa ukiwa Huna Kazi;

a) Mumeo
Mumea atakutesa jàmani. ASIJE akakudanganya Mtu kuwa ati atakupenda Miaka yôte huo ni Uongo. Upendo hauendi pàmoja na uvivu au utegemezi. Kadiri unavyomtegemea Mtu ndivyo Upendo wake unavyopungua na ndivyo chuki inavyoongezeka.

Mungu mwenyewe aliyekuumba hapendi úwe tegemezi Kwa Wengine.

b) Wakwe Zako
Mama Mkwe na mawifi. Watakuchukia vilivyo na wéwe mwenyewe utawachukia. Lazima wakutese na uteseke.
Utafulishwa manguo Ukweni mpaka ukome. Utatumwa vikazi Mshenzi Bila kujali umechoka au laah!
Ûkienda misiba ya Ukweni utamenyeka haswa Kwa sababu Huna lolote wewe. Huna Kazi wewe. Na Kwa nini usiteseke Wakati Huna lolote

c) Wanawake wanaomvizia Mumeo
Ukiwa MMA wa Nyumbani, golikipa hakika michepuko ya Mumeo wala haitakuogopa. Itakuletea dharau waziwazi na Hakuna lolote utafanya. Kwanza hata pesa ya kuhonga Polisi kimagendo wakamtie adabu mchepuko wa Mumeo Huna. Pesa za kutafuta Mganga mzuri wa kumloga mchepuko wako hauna. Yàani upoupo tuu kama MAITI. Nani akuogope wewe. Tunasema unakuwa nchi isiyo na Jeshi.

Wanawake wanaogopa kumchukua Mume wa mwanamke mwenzao mwenye Ñguvu za fedha au mwenye Mamlaka. Kwa Sababu Siku zote mwenye Pesa anaweza kufanya lolote.

NI kama Sisi Wanaume. Kama Huna Pesa Mkeo anaweza kuchukuliwa Muda wowote na usifanye Jambo lolote ukabaki kulaani tuu.

2. HUNA ELIMU YA UTAMBUZI
Kama Huna Elimu ya Utambuzi utateseka na kuteswa Sana ndàni ya Ndoa.
a) Lazima ujitambue wewe ni Mtu ili uweze kujiheshimu na kuheshimiwa Ûtu wako. Kazi ni kipimo cha Ûtu.

b) lazima ujitambue wewe ni Mwanamke hivyo lazima ujiheshimu kama Mwanamke.

Mwanamke anathamani yake. Lazima ujitunze ili uweze kutunzwa.

Siô wewe mwenyewe hata kujitunza Huwezi alafu utake Mumeo akutunze. Utateswa.

Lazima úwe Msafi. Nazungumzia Usafi wa Mwili na tàbia. Siô unalala na Wanaume wengi Kama Mbwa. Kîla Mwanaume akijisikia anakuja kumwaga takataka Zake kwèñye shimo Lako la taka. Uchi wako siô jalala.

Usishindane na Mwanaume UFUSKA. Mwenzako yeye huenda kumwaga uchafu wake kwèñye mashimo Huko wewe je, utamwaga uchafu au utamwagiwa matakataka.

Lazima ujitambue.

3. HUENDANI NA WAKATI
MTU yeyote asiyeendana na Wakati lazima Ndoa imtese. Hasa Mwanamke. Lazima ujue Dunia Ipo Wapi. Usikubali kupitwa na Wakati katika mambo ya Msingi. Zama hizi Wanawake nao wamepewa fursa ya kupata Elimu. Lazima uhakikishe nawe unaelimu angalau ya Diploma kama degree imekushinda.

Huu ni Wakati wa Elimu. Usipokuwa na Elimu ni kwamba HUENDANI na Wakati na Bila Shaka umepitwa na Wakati. Ndîo maana Shule zîpo Kila kata, ndîo maana vyuo kîla Siku vinajengwa. Elimu inakuongezea hadhi na thamani kwèñye jamii.

Mwanamke mwenye Elimu hawezi Kulingana hadhi na thamani na Yule Mwanamke asiye na Elimu.
Hata Ukweni unapoolewa ukiwa Huna Elimu hawawezi kukuchukulia wa Maana kivile. Jitahidi upate Elimu uendane na Wakati.

Siô uendane na Wakati Kwa mambo yasiyo na kichwa Wala miguu kama kukaa uchi, kwenda na mitindo ya Nguo. Sijui kusuka. Alafu Mbaya zaidi yôte hayo unategemea Mwanaume akufanyie. Huo ni kasongo Yeye.

Huu ni Wakati àmbao Wanawake wanafanya Kazi. Hilo nimeshaeleza. Mwanamke àmbaye anataka kukaa Nyumbani amepitwa na Wakati na Dunia lazima imshughulikie vilivyo.

Sisi Watibeli hatuwezi kuwa na Watu waliopitwa na Wakati hata wangekuwa Wazuri kama Malaika. Tunajua Hakuna mzuri àmbaye amepitwa na Wakati. Mzuri lazima ajitambue, Afanye Kazi, awe na Elimu Mbali na maumbile Yake.

4. HUWEZI KUMTOA OUT MUMEO NA KUMHUDUMIA

Kama hujui Kutoa Pesa ni wewe. Wanawake wengi Sana Siku hizi wakitoka out na Waume zao au familia hutoa Pesa na kufurahia na Waume na familia zào. Uliona Wapi mwanaume akamnyanyasa Mwanamke anayetoa Pesa ndàni ya familia na Kutoa familia out.

Hakuna Raha kama úwe na Mwanamke àmbaye wôte mna-share siô tuu penzi, miili Yenu, Hisia zenu, mawazo Yenu Bali pia hata pesa au mapato Yenu. Huyo ndîo Mkeo. Kama Mke hawezi kuchangia mapato ndàni ya familia Hapo Hakuna kitu Hapo. Huyo kapitwa na Wakati.

Kwanza sijawahi kuona Mwanamke anayeitwa Mke àmbaye yupo hivyo. Labda Makahaba waliojiingiza kwèñye Ndoa àmbao waô Mume ndîo kîla kitu anatakiwa kuhudumia. Na wengi huteseka na kuteswa.

Mwanamke mwenye uwezo wa kuhudumia familia Hana Muda wa Kufikiri mambo ya sijui ustawi wa Jamii sijui dawati la jinsia Kwa sababu anajua thamani yake.

Wanaume tunajua thamani zetu ndîo maana Kamwe hatuwezi kumpeleka Mwanamke dawati la jinsia sijui ustawi. Huko ni kujivua Ûtu. Tunajua Sisi tunahitaji zaidi. Tunamchango zaidi. Hivyo tukiona mambo hayaendi Sawa na tumejitahidi kuyaweka sawa tunafukuza.

Mwanamke anayejielewa hawezi kumpeleka Mtu ustawi wa Jamii Kisa matunzo ya Watoto wake aliowazaa yeye mwenyewe Wakati Mwanamke Husika anaweza kufanya Kazi na kujitunza na Kûtunza Watoto wake. Ikiwa alikuwa anatoa Pesa na kuchangia pato na Mumewe Kwa nini aone shida akiwa pekeake?.

Kwa ujumla Binti yàngu, Ndoa ni kwaajili ya Wanawake wanaoweza kujitegemea na siô Wanawake tegemezi.

Acha nipumzike sasa.
Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Wanaume hawajui wanataka mwanamke wa aina gani.. Akiwa mama wa nyumbani tegemezi wanasema ni mzigo hawamtaki tena. Akiwa mfanyakazi mwenye kipato chake pia hawamtaki ni malaya maana mawazo yao wanawake wanatoa unyumba maofisini. Kila upande una hasara na faida zake. Maisha hayana formula kila mtu aowe anayeona anamfaa. Kama wewe una uwezo wa kutunza familia yako mkeo akae nyumbani tu haina shida na ufunge domo lako usimwite mzigo. Na kama wewe unahitaji kusaidiwa mruhusu akafanye kazi, mwamini na kumpa uhuru usimsimange eti atakuwa anagawa naniliu huko ofisini; piga kimya maisha yaendelee.
 
Tegemezi atabaki tegemezi.
Maisha ya Mtu Yapo mikononi mwake mwenyewe ndîo maana Wanawake lazima wafanye Kazi.

Asifanye Kazi Siku mkiachana íwe Kwa talaka au Kifo Nani atamhudumia huyo Mwanamke?
Kama asipoanza tangu mwanzo kujitegemea lazima Dunia imnyooshe.
 
Mtibeli nakuelewa sana .
Inaonekana wewe ni msabato Kwa sababu wasabato wanasisitiza wanawake kufanya kazi Ili
A. Kuboost family economy.
B. Kutoa zaka na sadaka kutoka kwenye Pato la jasho lake
C. Kutokuwa tegemezi kwa mwanaume
D. Kuchangia maendeleo ya familia yake. mfano ujenzi nk
E. Kusimamia agizo la kila moja afanye kazi na asiyefanya kazi asile.
Nb. Mtibeli ukitaka kufurahia ndoa oa mwanamke msabato mwenye kazi utaishi maisha matamu na kufanya maendeleo makubwa .
Mwanamke msabato kipato chake ni cha familia . Wanawake wa kisabato hawana changu ni changu chako ni chetu .
 
Wanaume hawajui wanataka mwanamke wa aina gani.. Akiwa mama wa nyumbani tegemezi wanasema ni mzigo hawamtaki tena. Akiwa mfanyakazi mwenye kipato chake pia hawamtaki ni malaya maana mawazo yao wanawake wanatoa unyumba maofisini. Kila upande una hasara na faida zake. Maisha hayana formula kila mtu aowe anayeona anamfaa. Kama wewe una uwezo wa kutunza familia yako mkeo akae nyumbani tu haina shida na ufunge domo lako usimwite mzigo. Na kama wewe unahitaji kusaidiwa mruhusu akafanye kazi, mwamini na kumpa uhuru usimsimange eti atakuwa anagawa naniliu huko ofisini; piga kimya maisha yaendelee.
Sio kusaidiwa, ni mwanamke kujisaidia yeye mwenyewe.

Sio mume akikata motovau mkiachana mke anakua na maisha magumu, hata kulea wanao hawezi.

Mke awe anafanya kazi, binafsi sio mdau wa wale wamama wa nyumbani.
 
Mtibeli nakuelewa sana .
Inaonekana wewe ni msabato Kwa sababu wasabato wanasisitiza wanawake kufanya kazi Ili
A. Kuboost family economy.
B. Kutoa zaka na sadaka kutoka kwenye Pato la jasho lake
C. Kutokuwa tegemezi kwa mwanaume
D. Kuchangia maendeleo ya familia yake. mfano ujenzi nk
E. Kusimamia agizo la kila moja afanye kazi na asiyefanya kazi asile.
Nb. Mtibeli ukitaka kufurahia ndoa oa mwanamke msabato mwenye kazi utaishi maisha matamu na kufanya maendeleo makubwa .
Mwanamke msabato kipato chake ni cha familia . Wanawake wa kisabato hawana changu ni changu chako ni chetu .
Na mambo ya BALTHAZAR kwa mkeo huko maofisini uhakikishe unayafumbia macho...maana umemnadi mkeo kwa mikono yako mwenyewe.
 
Na mambo ya BALTHAZAR kwa mkeo huko maofisini uhakikishe unayafumbia macho...maana umemnadi mkeo kwa mikono yako mwenyewe.
Mkuu kwani hata akikaa nyumbani kama mwanamke ni malaya si bado kuna majirani, bodaboda, nk wanaweza tu kuwa wanajipigia? Au utamfungia ndani asitoke kabisa?
 
Back
Top Bottom