Dalili zinazoashiria magonjwa ya Afya ya Akili

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kihisia: Kukosa furaha na kuhuzunika sana. Au kuwa na furaha sana kupita kiasi wasiwasi na au woga kupita kiasi. Kupunguza kuongea au kutokuongea kabisa au kuongea sana kupita kiasi. Hasira za haraka haraka hata kufikia kupiga wengine. Kuwa na msongo wa mawazo. Kujitenga na watu na kupenda kukaa mwenyewe muda mwingi au kupenda kuwa na watu sana kuliko kawaida. Kutokuwa na ari ya kufanya kazi au kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja bila ya kuzikamilisha. Kutokuonesha hisia yoyote usoni mwake (mf. furaha au huzuni nk). Kutokujijali usafi na mwonekano wake. Kuhisi maisha hayana thamani na kuona bora kufa kuliko kuishi na hatimaye kufikia uamuzi wa kujiua na hata kuua wengine.

Kimwili: Mwili kukosa nguvu au kuhisi mwili una nguvu sana kupita kiasi. Kukosa usingizi au kulala usingizi sana kupita kiasi. Kukosa hamu ya kula au kuwa na hamu sana ya kula. Kutokutulia (kuhamanika) au kutulia sehemu moja muda mrefu bila ya kujisogeza. Maumivu sehemu mbalimbali za mwili kama vile kichwa, mabega, mgongo, na viungo mbalimbali ambavyo akienda hospitali vipimo havionyeshi tatizo lolote la kimwili.

Kiakili: Kukosa umakini wa shughuli zake za kila siku. Kusahau kwa haraka au kupoteza kumbukumbu. Kukosa uwezo wa kupambanua mambo kwa mitazamo tofauti. Kusikia sauti ambazo hazipo na kuona vitu ambavyo havipo. Imani ya ajabu ambazo haziendani na mila, imani au desturi za jamii yake; kama vile yeye ni mtu maarufu, au anaamini kuwa yeye ni nabii. au anaamini kupokea taarifa kutoka kwenye redio au mitandao ya simu. Pia anaamini ana nguvu ya ziada kutoka nje ya mwili wake inayomsababishia kutenda au kuwaza mambo anayoyawaza. Anaamini mawazo yake yanapunguzwa au kuongezwa na watu wasiojulikana, vyombo vya habari kama vile Radio na TV kuwa vinamzungumzia yeye, au vinaongea mawazo yake yeye. Mawazo yake hayana mtiririko unaoeleweka.

Baadhi ya aina za magonjwa ya akili ni kama vile: Magonjwa ya kuchanganyikiwa (Psychoses), magonjwa yanayohusiana na matumizi mabaya ya pombe na uraibu wa dawa ya kulevya; magonjwa yanayohusiana na matumizi ya pombe, uraibu wa dawa ya kulevya (addiction of alchohol and drugs). Aidha kuna Magonjwa ya wasiwasi au hofu/woga (anxiety/Phobia), magonjwa yanayoathiri hisia (mood disorders) ambayo hupelekea watu kujiua pamoja na matatizo ya jinsia (sexual dysfuctions). Magonjwa haya mara nyingi yanapoanza yanaonekana ni hali ya kawaida tu na huenda pasiwepo na jitihada yoyote ya kupata msaada wa kitabibu hadi hali itakapokuwa mbaya au kuzidiwa. Pia watoto nao huwa wanaugua magonjwa ya akili ambayo kama yasipotambuliwa na kupatiwa matibabu mapema huathiri ukuaji wao pamoja na uwezo wao wa kupata elimu.

Vipo visababishi vingi ambavyo hupelekea matatizo ya afya ya akili, sababu hizi ni: za kijamii na kisaikolojia kam vile umaskini uliokithiri, kutengwa na jamii, kuwa tegemezi, upweke na upotevu wa vitu mbalimbali (mfano kufiwa na mtu wa karibu, kupoteza mali, kupoteza kazi au kupata ulemavu), mafarakano na mipasuko katika jamii pamoja na matatizo ya mahusiano, kukosa huduma muhimu, unyanyapaa, unyanyasaji na ubaguzi wa aina mbalimbali. Aidha kuna sababu nyingine za kibayolojia kama vile mtoto kupata shida wakati wa kuzaliwa na kusababisha mgandamizo wa ubongo, uchungu wa muda mrefu na mtoto kukosa hewa ya oksijeni, maradhi kwa mama mjamzito ambayo hushambulia mfumo wa fahamu wa mtoto aliye tumboni na pia kama wazazi wana vinasaba vya ugonjwa wa akili mtoto/watoto pia wanaweza kurithi.

Wagonjwa wa afya ya akili wanahitaji uangalizi na matunzo maalum ya kitaalam; pamoja na ukweli huo, huduma ya afya ya akili hazipatikani kwa urahisi katika vituo vya afya na zahanati, Ili kuboresha huduma hizo na haswa katika kutoa huduma za matibabu kwa kuzingatia utu wa wagonjwa wa akili, serikali zishirikiane na wadau mbalimbali ili kutoa mafunzo maalum ya namna ya kuwahudumia wagonjwa wa akili; kwa kuheshimu na kujali utu wa wagonjwa hawa. Watumishi wa afya wapewe mafunzo maalum ya namna ya kuwahudumia wagonjwa wa akili, hii ikiwa ni pamoja na kuheshimu utu wa wagonjwa, kuwaelimisha wagonjwa pamoja na ndugu zao kuhusu magonjwa ya akili na matibabu yake pamoja na kuwashirikisha katika maamuzi ya matibabu na kupata ridhaa kutoka kwao.
 
Ukifuatilia .. matatizo ya akili yamekithiri kwenye jamii zetu..
 
Asante ndugu mtaalamu. Vipi na hao wanaoamka mapemaaa, wanavaa vizuri, wanakwenda kazini kukata umeme tu? Hizo siyo dalili hizohizo?
Yaani hapo haina hata kuuliza wale na wa idara ya maji nadhani haina haja ya vipimo. Hawana akili sawa sawa.
 
Hii ikimfikia Ummy Mwalimu nadhani ataelewa kwanini watu wanaomba uhamisho,halafu yeye anazuia huku akitabasamu tu utazani ni vizuri,wanalazimisha watu wafanye kazi huku wanastress mwanzo mwisho.
 
Unaweza kujitambua kuwa una tatizo kwa dalili zilizo tajwa kwenye hili andiko au hauwezi hata kama kuna dalili kadha zinakugusa lakini bado ukajiona si miongoni mwao?
 
Kihisia: Kukosa furaha na kuhuzunika sana. Au kuwa na furaha sana kupita kiasi wasiwasi na au woga kupita kiasi. Kupunguza kuongea au kutokuongea kabisa au kuongea sana kupita kiasi. Hasira za haraka haraka hata kufikia kupiga wengine. Kuwa na msongo wa mawazo. Kujitenga na watu na kupenda kukaa mwenyewe muda mwingi au kupenda kuwa na watu sana kuliko kawaida. Kutokuwa na ari ya kufanya kazi au kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja bila ya kuzikamilisha. Kutokuonesha hisia yoyote usoni mwake (mf. furaha au huzuni nk). Kutokujijali usafi na mwonekano wake. Kuhisi maisha hayana thamani na kuona bora kufa kuliko kuishi na hatimaye kufikia uamuzi wa kujiua na hata kuua wengine.

Kimwili: Mwili kukosa nguvu au kuhisi mwili una nguvu sana kupita kiasi. Kukosa usingizi au kulala usingizi sana kupita kiasi. Kukosa hamu ya kula au kuwa na hamu sana ya kula. Kutokutulia (kuhamanika) au kutulia sehemu moja muda mrefu bila ya kujisogeza. Maumivu sehemu mbalimbali za mwili kama vile kichwa, mabega, mgongo, na viungo mbalimbali ambavyo akienda hospitali vipimo havionyeshi tatizo lolote la kimwili.

Kiakili: Kukosa umakini wa shughuli zake za kila siku. Kusahau kwa haraka au kupoteza kumbukumbu. Kukosa uwezo wa kupambanua mambo kwa mitazamo tofauti. Kusikia sauti ambazo hazipo na kuona vitu ambavyo havipo. Imani ya ajabu ambazo haziendani na mila, imani au desturi za jamii yake; kama vile yeye ni mtu maarufu, au anaamini kuwa yeye ni nabii. au anaamini kupokea taarifa kutoka kwenye redio au mitandao ya simu. Pia anaamini ana nguvu ya ziada kutoka nje ya mwili wake inayomsababishia kutenda au kuwaza mambo anayoyawaza. Anaamini mawazo yake yanapunguzwa au kuongezwa na watu wasiojulikana, vyombo vya habari kama vile Radio na TV kuwa vinamzungumzia yeye, au vinaongea mawazo yake yeye. Mawazo yake hayana mtiririko unaoeleweka.

Baadhi ya aina za magonjwa ya akili ni kama vile: Magonjwa ya kuchanganyikiwa (Psychoses), magonjwa yanayohusiana na matumizi mabaya ya pombe na uraibu wa dawa ya kulevya; magonjwa yanayohusiana na matumizi ya pombe, uraibu wa dawa ya kulevya (addiction of alchohol and drugs). Aidha kuna Magonjwa ya wasiwasi au hofu/woga (anxiety/Phobia), magonjwa yanayoathiri hisia (mood disorders) ambayo hupelekea watu kujiua pamoja na matatizo ya jinsia (sexual dysfuctions). Magonjwa haya mara nyingi yanapoanza yanaonekana ni hali ya kawaida tu na huenda pasiwepo na jitihada yoyote ya kupata msaada wa kitabibu hadi hali itakapokuwa mbaya au kuzidiwa. Pia watoto nao huwa wanaugua magonjwa ya akili ambayo kama yasipotambuliwa na kupatiwa matibabu mapema huathiri ukuaji wao pamoja na uwezo wao wa kupata elimu.

Vipo visababishi vingi ambavyo hupelekea matatizo ya afya ya akili, sababu hizi ni: za kijamii na kisaikolojia kam vile umaskini uliokithiri, kutengwa na jamii, kuwa tegemezi, upweke na upotevu wa vitu mbalimbali (mfano kufiwa na mtu wa karibu, kupoteza mali, kupoteza kazi au kupata ulemavu), mafarakano na mipasuko katika jamii pamoja na matatizo ya mahusiano, kukosa huduma muhimu, unyanyapaa, unyanyasaji na ubaguzi wa aina mbalimbali. Aidha kuna sababu nyingine za kibayolojia kama vile mtoto kupata shida wakati wa kuzaliwa na kusababisha mgandamizo wa ubongo, uchungu wa muda mrefu na mtoto kukosa hewa ya oksijeni, maradhi kwa mama mjamzito ambayo hushambulia mfumo wa fahamu wa mtoto aliye tumboni na pia kama wazazi wana vinasaba vya ugonjwa wa akili mtoto/watoto pia wanaweza kurithi.

Wagonjwa wa afya ya akili wanahitaji uangalizi na matunzo maalum ya kitaalam; pamoja na ukweli huo, huduma ya afya ya akili hazipatikani kwa urahisi katika vituo vya afya na zahanati, Ili kuboresha huduma hizo na haswa katika kutoa huduma za matibabu kwa kuzingatia utu wa wagonjwa wa akili, serikali zishirikiane na wadau mbalimbali ili kutoa mafunzo maalum ya namna ya kuwahudumia wagonjwa wa akili; kwa kuheshimu na kujali utu wa wagonjwa hawa. Watumishi wa afya wapewe mafunzo maalum ya namna ya kuwahudumia wagonjwa wa akili, hii ikiwa ni pamoja na kuheshimu utu wa wagonjwa, kuwaelimisha wagonjwa pamoja na ndugu zao kuhusu magonjwa ya akili na matibabu yake pamoja na kuwashirikisha katika maamuzi ya matibabu na kupata ridhaa kutoka kwao.
Paragraph ya kwanza ni bipolar
 
Back
Top Bottom