Damas Nbumbaro: Rais Samia ameagiza mtumishi yeyote wa umma ambaye ndiye chanzo cha migogoro mimi nihangaike naye

Damas Nbumbaro: Rais Samia ameagiza mtumishi yeyote wa umma ambaye ndiye chanzo cha migogoro mimi nihangaike naye

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, ametoa ujumbe mkali kwa watumishi wa umma wanaosababisha migogoro kwa kuwadhulumu wananchi, akisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Akizungumza siku ya Jumanne, Machi 4, 2025, katika Uwanja wa TBA, Arusha, wakati wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, Ndumbaro amesema kuwa serikali imekuja na timu ya wanasheria zaidi ya 50, pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, ili kusaidia wananchi kupata haki zao.

Ndumbaro amesisitiza kuwa Rais Samia ameagiza hatua zichukuliwe dhidi ya watumishi wa umma wanaosababisha mateso kwa wananchi kupitia migogoro ya ardhi na masuala mengine ya haki za kiraia.

"Samia ameagiza mtumishi yeyote wa umma ambaye ndiye chanzo cha migogoro mimi nihangaike naye. Ewe mtumishi wa umma ambaye umekuwa chanzo cha kuwadhulumu wananchi wanyonge, arobaini zako zimefika. Samia ameandaa dawa ya kwako, imechemka, imeiva, nimekuja kukunywesha," amesema kwa msisitizo.

Ameongeza kuwa baadhi ya migogoro itaweza kutatuliwa ndani ya siku nane, huku mingine ikiendelea kushughulikiwa na wataalamu wa sheria waliopangwa kusimamia kesi hizo bila malipo kwa wananchi, kwa gharama zote kubebwa na Rais Samia.

Ndumbaro ameelezea kuwa kampeni hii ni moja ya hatua zinazodhihirisha uongozi wa Rais Samia kama mwanamke anayejali haki za wananchi wanyonge.

"Tumezoea wananchi ndio wanawatafuta wanasheria, lakini kwa Samia, wanasheria ndio wanawatafuta wananchi. Hii ndiyo faida ya kuwa na Rais mwanamke. Sisi wanaume tunapenda kufikiria mambo makubwa sana, wenzetu wanawake wanafikiria zaidi maendeleo ya jamii, haki za binadamu, na watu wasiokuwa na uwezo," amesema.


 
Back
Top Bottom