Damian Marley Atukanwa na Mwanahabari Kenya

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
854
Mtoto wa Mfalme wa Reggae duniani, Damian Marley au Junior Gong, ametukanwa na mwanahabari uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, baada ya Damian kukataa kupiga picha 'selfie'.

Mwanahabari huyo ambaye alionekana kutokuwa na maadili alianza kumtukana Damian, kitu ambacho kimezua mjadala mkubwa Kenya juu ya luugha chafu ya mwanahabari huyo. Katika mitandao ya kijamii ya nchini Kenya, watu wengi wamelaani kitendo hicho cha mwanahabari huyo, na wengine kwenda mbali zaidi kwa kutaka achukuliwe hatua kwa kuwa mfano mbaya kwa media house yake.
gonga link hii
Damian Marley Abused By Journalist At Airport In Kenya After Refusing To Take A Selfie
 

Attachments

  • damianmarley.jpg
    47.8 KB · Views: 65
Yaani uanlazimisha selfie na mtoto wa Bob, je angekuwepo kipindi cha BOB mwenyewe na kunyimwa selfie nae si angejinyonga huyu?! Mpuuzi kwelikweli.
 
Yaani uanlazimisha selfie na mtoto wa Bob, je angekuwepo kipindi cha BOB mwenyewe na kunyimwa selfie nae si angejinyonga huyu?! Mpuuzi kwelikweli.
Mwasu,baadhi ya watu tunashindwa kutambua kwamba, hata celebrities ni binadamu kama walivyo wengine. Kwamba, si kila wakati atafanya kile unachotaka. Kuna wakati naye hajisikii kuwa kwenye hali fulani.
 
CHA The GREAT
Kisa eti amekataliwa kupiga naye picha.... ahaaa haaa haaa.
Sisemi mengi ili nisije nikazua mengi buree.
 
Huyo junia gong ni mpumbavu!!!
Fans ndio wanamfanya aelee kwenye boti ya sanaa kwenye bahari ya burudani!!! Sasa kujipa maujiko ya kurithi ni ulimbukeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…