KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Kipindi cha miezi kadhaa iliyopita mwaka huu, Mimi kama mkazi wa hili eneo, niliandika hapa juu ya Dampo ambalo siyo rasmi lililoanzishwa na Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu katikati ya makazi yetu.
Dampo hili ambalo lipo mtaa wa Kidinda, Halmashauri hii ya Mji wa Bariadi, maeneo ya Majengo karibu na Makaburi, lilikuwa hatari kwa Afya zetu na kwa maisha yetu.
Tunashukuru JamiiForums kwa kutusaidia kupaza sauti sisi wananchi wa mitaa hiyo, hili Dampo lilitutesa sana, tulikuwa kwenye hatari kubwa, harufu Kali ndiyo ilikuwa hatari kubwa sana kwetu, inzi Kila wakati hatukupata furaha ya chakula kwenye majumba yetu.
Baada ya kupaza sauti hapa, Uongozi wa Halmashauri ulianza kuchukua hatua, na kulifunga rasmi Dampo hilo na kuzuia watu wasiendelee kutupa taka.
Matangazo yaliwekwa yalieleza Dampo hilo kufungwa, lakini Pia tunashuru Halmashauri kwa kuwazuia wale wazoa taka Binafsi kwenye makazi ya watu ambao ndiyo walikuwa chanzo cha uwepo wa Dampo hili, kwani walikusanya uchafu huo na kuja kutupa eneo hili.
Baada ya wazoa taka hao kuzuiwa, Dampo kwa sasa limeanza kutoweka taratibu na adha ambao tulipata hapo awali kwa sasa imepungua kwa kiasi kikubwa.
Sasa Naomba kuleta hii hoja hapa, nayo tusaidiwe, hili eneo ambalo Dampo lilianzishwa ni eneo la Makaburi, ni eneo la kuhifadhi ndugu, jamaa na watu wetu wa karibu ambao wametangulia mbele ya Haki.
Hoja hapa ni kuwa, Kuna baadhi ya wananchi hatujui kama wanatoka kwenye huu mtaa wetu au wanatoka mitaa mwingine ya Mji wa Bariadi, wamekuwa wakileta uchafu wao na kuendelea kutupa hili eneo.
Jambo hili limeanza kidogo kidogo, lakn kadri siku zinavyokwenda linaongezeka kidogo kidogo, Kuna baadhi ya watu nadhani ni nyakati za usiku, wanaendelea kuleta uchafu hapa na kutupa.
Uchafu huo umesambaa hadi kwenye makaburi, wanajua Dampo limeuziliwa, lkn kwa kuwa ulibaki uchafu kidogo, wao wamechukulia hiyo kama fursa ya kuendelea kuleta uchafu kidogo kidogo.
Na wengi wanaoleta ni wale wananchi wenyewe na Wala siyo wale wazoa uchafu kama zamani, maana hao tyr wamedhibitiwa, lkn Hawa ambao wanaendelea kuleta huu uchafu sasa wanaongezeka kidogo kidogo.
Hatua ambazo Halmashauri ilizichukua uko nyuma baada ya sisi kupiga kelele hapo awali, tunaomba izichukue katika hili kwa hawa ambao wanaoleta uchafu wamejificha.
Tunaomba hili lichukuliwe hatua haraka, kwani bila ya kufanya hivyo Dampo litarejea kama ilivyokuwa awali, tunaomba ulinzi uwekwe ili kubaini hawa wanaoendelea kufanya hivi.
Pia Soma:
~ Simiyu: Baada ya kulalamika Dampo kwenye makazi ya watu, viongozi watoa tangazo la kuzuia Dampo lakini waweka kifaa cha kuhifadhi taka
~ Halmashauri ya Bariadi yaanzisha Dampo katikati ya makazi ya Wananchi