A
Anonymous
Guest
Tumepeleka malalamiko yetu kwa Mwenyekiti wa Mtaa mara nyingi tu lakini hatuoni utekelezaji wowote wa kusitisha. Huu ni mwaka wa pili tangu dampo hilo lianzishwe, kuna muda tukipiga kelele wanasimama kidogo kisha baada ya muda wanaendelea kama kawaida.
Malalamiko hayo tumeshafikisha hadi kwa Mbunge wetu lakini hakuna alichofanya.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) fikeni eneo hilo, wakazi wa maeneo hayo tuna hali mbaya, tunapoelekea kuna uwezekano wa kuibuka kwa mlipuko wa magonjwa mbalimbali kutokana na uchafu uliopo.