Danadana: Kesi ya Kabendera yaahirishwa kwa madai kwamba Hakimu kapata udhuru

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mahakama imeshindwa kusoma kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa haba ( 348 X 640 ).jpg

Kesi hii ya Uhujumu uchumi ambayo ilibadilishwa kutoka kwenye tuhuma za uraia leo imeshindwa kuendelea kwa vile Mh Hakimu ameamua kutokufika Mahakamani .

Imepangwa kuendelea tarehe 24 February.

======

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa habari wa Tanzania, Erick Kabendera imekwama kuendelea katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya hakimu anayeisikiliza, Janeth Mtega kupata udhuru.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kutakatisha Sh173 milioni.

Leo Jumatatu Februari 17, 2020 ni mara ya pili kesi hiyo kuahirishwa ndani ya wiki moja. Februari 10, 2020 kesi hiyo iliahirishwa baada ya upande wa mashtaka kuomba mahakamani hiyo ipange tarehe inayofuata yaani Februari 11, 2020.

Februari 11, 2020 upande wa mashtaka uliomba mahakama hiyo kuahirisha ili mshtakiwa apate nafasi ya kukutana na mawakili wa Serikali kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa kumaliza kesi yake.

Leo wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon ameieleza mahakama hiyo kuwa hakimu anayesikiliza kesi hiyo amepata udhuru na kuomba mahakama kuahirisha kesi hiyo.

Simon ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu mkazi, Vicky Mwaikambo wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

"Kesi hii ilikuja kwa ajili ya kutajwa na hakimu anasikiliza kesi hii amepata udhuru, naomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na shauri hili,” amedai wakili Simon.

Simon baada ya kueleza hayo Reginald Martin ambaye ni wakili wa Kabendera aliomba mahakama ipange tarehe fupi kwa sababu wapo katika hatua za mwisho kukamilisha makubaliano ya kumaliza kesi hiyo.

Hakimu Mwaikambo baada ya kusikiliza hoja za upande zote, ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 24, 2020.

Kabendera amerudishwa rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha linalomkabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

Kwa mara ya kwanza alifikishwa Kisutu Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha Sh173.2 milioni.

Chanzo: Mwananchi
 
Huu uwajibikaji maofisini unaohubiriwa kurejeshwa kwa kasi ya mwewe huko mahakamani vp?

Maanake moja ya mafanikio ya awamu ya tano ktk hutuba nyingi ni hili swala la uwajibikaji wa watumishi wa umma, sasa huko mahakani vp?

Hakuna hakimu mwingine kushikiliza shauri hilo?

Ikitokea hakimu huyo kaugua na may be kafa kesi hiyo inakuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesi hii ya Uhujumu uchumi ambayo ilibadilishwa kutoka kwenye tuhuma za uraia leo imeshindwa kuendelea kwa vile Mh Hakimu ameamua kutokufika Mahakamani .

Imepangwa kuendelea tarehe 24 February.
Kuwa na subra kamanda,hakimu pia ni binadamu kama wewe,kwani kabendera ni papai mpaka uogope litaoza kwa kukaa ndani
 
Kesi ngapi huwa zinaahirishwa kila siku ndio iwe kesi hii?
Kitu ninacho mpendea Mungu ni kwamba aliweka KIFO, kifo kipo kwa washenzi hata na waungwana, matajiri na mafukara, maadui zetu na hata ndugu na Rafiki zetu, watesi na wateswa sote tutakufa one day; hili jambo hua linanifanya NIPENDE kutenda wema na kujitahidi kupunguza CHUKI isiokua na sababu kwa watu hata kwa maadui zangu ikibidi. Asante Mungu kwa huo USAWA
 
Kwa hiyo?
 
Huyu akili itamkaa sawa tu,alijifanya joloe mwiti ,akanasa

Kesi hii ya Uhujumu uchumi ambayo ilibadilishwa kutoka kwenye tuhuma za uraia leo imeshindwa kuendelea kwa vile Mh Hakimu ameamua kutokufika Mahakamani .

Imepangwa kuendelea tarehe 24 February.

======

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa habari wa Tanzania, Erick Kabendera imekwama kuendelea katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya hakimu anayeisikiliza, Janeth Mtega kupata udhuru.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kutakatisha Sh173 milioni.

Leo Jumatatu Februari 17, 2020 ni mara ya pili kesi hiyo kuahirishwa ndani ya wiki moja. Februari 10, 2020 kesi hiyo iliahirishwa baada ya upande wa mashtaka kuomba mahakamani hiyo ipange tarehe inayofuata yaani Februari 11, 2020.

Februari 11, 2020 upande wa mashtaka uliomba mahakama hiyo kuahirisha ili mshtakiwa apate nafasi ya kukutana na mawakili wa Serikali kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa kumaliza kesi yake.

Leo wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon ameieleza mahakama hiyo kuwa hakimu anayesikiliza kesi hiyo amepata udhuru na kuomba mahakama kuahirisha kesi hiyo.

Simon ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu mkazi, Vicky Mwaikambo wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

"Kesi hii ilikuja kwa ajili ya kutajwa na hakimu anasikiliza kesi hii amepata udhuru, naomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na shauri hili,” amedai wakili Simon.

Simon baada ya kueleza hayo Reginald Martin ambaye ni wakili wa Kabendera aliomba mahakama ipange tarehe fupi kwa sababu wapo katika hatua za mwisho kukamilisha makubaliano ya kumaliza kesi hiyo.

Hakimu Mwaikambo baada ya kusikiliza hoja za upande zote, ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 24, 2020.

Kabendera amerudishwa rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha linalomkabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

Kwa mara ya kwanza alifikishwa Kisutu Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha Sh173.2 milioni.

Chanzo: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu pekee tunaobadilika badilika zaidi na kutokutabirika ni sisi huku Tz
 
Back
Top Bottom