Insidious
JF-Expert Member
- Oct 28, 2020
- 654
- 895
Napenda kutoa malalamiko yangu makali na kero kuhusu kucheleweshwa kwa malipo ya fidia kwa ardhi tuliyotoa KIPUNGUNI kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa serikali. Taarifa ya tathmini ya ardhi ilifanywa tangu jana, na hata miaka ya nyuma (1997), lakini hadi leo hatujaona malipo yoyote.
Yalishatolewa matamko kutoka kwa mawaziri wawili (Mwigulu na Mbarawa) tena wakiwa bungeni, waliotoa ahadi hewa pamoja na mbunge wa segerea (bonnah kamoli) kuwa malipo yatafanyika mwaka huu, wakihakikisha yatafanyika mwezi huu wa nane ambao bado siku sita tu uishe.
Naomba malipo yafanyike mara moja ili tuweze kuhama kwenda maeneo bora zaidi, kwani haturuhusiwi kuendeleza chochote kattika maeneo haya ambayo sasa yamekuwa vichaka.
Aidha, tunasisitiza kwamba malipo haya yawe na riba kama ilivyoainishwa katika sheria za upatikanaji wa ardhi.
Tunahitaji hatua za haraka kuchukuliwa ili kuhakikisha tunapata haki yetu.
Pia soma:Mbunge Bonna Kamoli atishia bungeni sakata la wananchi Kipunguni kupisha Airport, hawajalipwa fidia miaka 27 sasa