Dangote: Nikiinunua Arsenal nitamfuta Wenger

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Mfanyabiashara tajiri raia wa Nigeria Aliko Dangote, ambaye anaorodheshwa kuwa mtu tajiri zaidi Afrika, amesema kuwa atamfuta kazi meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ikiwa atafaulu kuinunua klabu hiyo ya Uingereza, kwa mujibu wa shirika la Bloomberg.

Wakati wa mahojiano na shirika hilo, Bwana Dangote alisema kuwa atajaribu kununua klabu hiyo, wakati ujenzi wa kiwanda chake cha kusafisha mafuta cha gharama ya dola bilioni 11 mjini Lagos utakamilika.

Bw. Dangote anasema amekuwa shabiki wa Arsenal tangu miaka 1980.

Wenger ni mmoja wa mameneja wa kandanda wanaosifika sana barani Ulaya na hivi majuzi, alisaini mkataba wa miaka miwili na kuendelea kuwa na klabu hiyo kwa zaidi ya miongo miwili.

Kuna maoni tofauti kutoka kwa wafuasi wake, wengine wakisema kuwa klabu hiyo inahitaji meneja mpya ili kiweze kurejea hadhi yake.

Chanzo: BBC Swahili
 
ni hapo prez Mo Buhari atakapom-Manji huyo Dangote ..sijui Arsenal watakuwa wageni wa nani?
 
Binafsi napenda sana hainunue arsenal kwa sababu napenda mafanikio,,ila tatizo linakuja kwamba...Wazungu watakubali kumuuzia timu mwafrika!!!lakini yote yanawezekana ngoja tuvute subila..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…