Daniel Chongolo, anza na haya mambo ili kuepuka usaliti wa Bashiru

Daniel Chongolo, anza na haya mambo ili kuepuka usaliti wa Bashiru

KooZito

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2020
Posts
397
Reaction score
1,377
Wanabodi, hili andiko ni kutoka kwa Mwandishi Nguli Bollen Ngetti FaceBook page yake. Naisukuma kwenu.
_____________________

Daniel Chongolo, anza na haya kuepuka usaliti wa Bashiru

Na Bollen Ngetti

KWAMBA Katibu Mkuu mpya wa CCM Ndugu Daniel Chongolo ni mtu sahihi kwa nafasi hiyo, halina ubishi wowote. Chongolo ni rafiki yangu, ninamfahamu umakini wake na utendaji wake.

Daniel ni miongoni mwa vijana waliokulia na kulelewa na chama. Hatujawahi kusikia makando-kando yake. Ni mcha Mungu lakini hodari kwa mikakati ya ushindi katika chaguzi. Si Msemaji sana majukwaani lakini hodari na makini kiutendaji shughuli za chama.

Siku nyingine nitaandika wasifu wake na huo uhodari wake unatokana na nini. Kwa hakika Mwenyekiti SSH amemleta mtu sahihi kwa CCM.

Hata hivyo nitumie ukuta huu kumshauri mambo kadhaa kwa aina ya chama aliyokabidhiwa kama Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa. Haya nitakayosema pengine yakawa machungu lakini akikubali kuyameza ataokoa chama.

MOSI: Chongolo umepokea chama kilichokuwa kimepasuka mapande mapande. Ni chama kilichokuwa na kundi linalojiita "alwatan" yaani wanaoamini kukijua chama hicho ndani nje lakini wakiwa wamesukumwa pembeni wasisikilizwe.

Hawa ni "vijana wa zamani" ambao mchango wao ndani ya CCM si wa kubeza. Hawakusikilizwa na kundi la pili lililojibatiza "CCM Mpya" lakini kimsingi hawakijui chama zaidi ya kukariri Manifesto ya chama.

Ni genge jipya lililokuwa na kauli mbiu, "it's our time to eat". Limekuwa ni genge hatari sana kwa mustakabali wa demokrasia mchini.

Kama ulisikia watu wakitekwa, kuteswa, kupotezwa, kufilisiwa, kudhihakiwa kiliendeshwa na CCM Mpya kwa kushirikiana na "wasiojulikana". Ndilo genge lililoratibu matokeo ya Uchaguzi 2019/2020 kwa kutumia nguvu ya mitulinga.

Genge la tatu ni "gweregwere" yaani wakimbizi wa kiuchumi waliovihama vyama vyao na kujiunga na CCM kusaka malisho. Genge hili lilishindwa kuishi na makundi mawili ya hapo juu nalo likajiundia himaya yao hata kama halikufua dafu. Limeyeyuka kiaina!

Kazi ya kwanza ni kuyaunganisha makundi haya kuwa wamoja ndani ya chama ili kila mmoja ajihisi sehemu ya chama. Kila mmoja ajihesabu ni mwana-CCM kwa uhuru.

Kazi nyingine ni kuiweka hadharani ripoti ya uchunguzi wa mali za chama iliyoongozwa na Dk. Bashiru Ally. Hii ripoti ndio imetumika kama rungu la chuma kuponda vichwa vya yeyote aliyehoji utendaji wa Serikali. Iwe public document maana imetumia mamilioni fedha za walipa kodi. (Nitalifafanua next time). Ropoti hii imefichwa sana maana ni rungu ambapo ulipohoji jambo uliitwa na kuoneshwa page inayokuhusu kisha kuambiwa, "wewe ni mhujumu uchumi twende Kisutu au kaa kimya tukusamehe?" Kwa kuwa tuliogopa kesi hiyo ungekaa tu kimya na kuufyata.

Eneo lingine ni uhusiano wetu na nchi ya Sahara Magharibu. Hii nchi inakaliwa kwa mabavu na Morocco. Miaka yote vyama vyote vya ukombozi vikiongozwa na CCM viliunga mkono harakati za Polisario ili nchi hii iwe huru. Hatua hii iliifanya Morocco iondolewe uanachama OAU sasa AU.

Baada ya CCM Mpya kuingia madarakani Magufuli akiwa M/Kiti wa AU alitumia "uhusiano wake" na Mfalme wa Morocco na CCM Mpya pekee Kati ya vyama 6 ikaunga mkono Morocco kukalia kwa mabavu Sahara Magharibu kwa zawadi ya "tende" ya kujengewa uwanja wa mpira Dodoma. Hili halikubaliki na linamtoa machozk Mwl. Nyerere kaburini na Mkapa.

CCM ivunje uhusiano huu katili ili kusaidia Polisario kupigania Uhuru wa Sahara Magharibi. Rejea vita vya ukombozi kusini mwa Afrika. Wenzetu wanatushangaa! Kwa leo niishie hapo. Nitakuja baadaye.

Ndimi mjoli wenu.
BollenNgetti@2021
0683 226539
 
Back
Top Bottom