Ni simanzi,majonzi yasiyo na kifani kwetu wote Watanzania tuliofamu ndugu yetu Kabisi,
Kwetu tuliobahatika kuwa naye chuoni Makerere
Kwetu zaidi wana LUMBOX solidarity na Lumumbists kwa pekee.
Binafsi nilibahatika kuwa nae kwa ukaribu zaidi pale LUMUMBA Hall kwa mda wa miaka miwili na hata kusoma nilikuwa nasomea chumbani kwake kwani palikuwa na mazingira ya utulivu, mpangilio mzuri na kwa kweli ni sikitiko kubwa sana kwangu binafsi
Tulivumilia mengi sana,migomo ya kila mara pale,chakula kibovu mess,tear gas,kukimbizwa na askari wakati wa migomo,matatizo ya kukosa maji mara kwa mara pamoja na kuibiwa vifaa vya eletronics kama redio na TV tulipokuwa likizo.
KABISI alikuwa mcheshi si kwa Watanzania wenzake tu bali naamini,viongozi wa LUmumba Hall tukianza na Warden,custodians,wapishi,wafanya usafi pamoja na majirani wa LUMBOX SOLIDARITY
Kama si jitihada na msimamo dhabiti wa ndugu yetu KABISI (TAZAMA) chama cha wanafunzi MUK na Mbarara UN kisingelikuwa na nguvu yoyote
Upatikanaji wa vyumba
Ela ya kujikimu kutoka bodi ya mikopo
Kwa ujumla Dani alikuwa mtetezi wa maslahi yetu chuoni
Nasikitika sana nyota iloanza kuchomoza imetokomea kabla ya walio wengi kufaidika
Sie tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi na kazi ya mola haina makosa
Kwa wale wanafuatilia huu msiba kwa karibu tunaomba mtujulishe yanayojiri