Daniel Sillo: Uhamiaji ongezeni kasi ili watu wapate Vitambulisho vya NIDA

Daniel Sillo: Uhamiaji ongezeni kasi ili watu wapate Vitambulisho vya NIDA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo amezitaka Idara mbili zilizopo chini ya Wizara yake ambazo ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera kushirikiana ili kuboresha utendaji kazi.

Kauli hiyo ameitoa Wilayani Muleba Mkoani Kagera katika Mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi ambapo amewataka kushirikiana na kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuwezesha upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wakati.

"Niwaombe Uhamiaji na NIDA shirikianeni katika suala zima la utambuzi na usajili wa wananchi ili kuharakisha upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa kwa Wananchi wenye sifa. Sitegemei kuona jambo lolote kukwamisha Vitambulisho hivyo bila sababu za msingi," amesema Sillo.

Soma Pia: NIDA badilikeni na toeni huduma kwa weledi

Ametoa agizo hilo ikiwa ni maelekezo ya Katibu Mkuu wa Chama akiwa Wilayani Ngara Mkoani Kagera na kuelezwa na Wananchi kuwa bado wanachangamoto ya upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa.

Hata hivyo, amemuelekeza Afisa usajili wa NIDA kuwa katika Mkoa wa Kagera bado kuna Vitambulisho 78,766 havichukuliwa na Wananchi ambapo ametoa wito kwa Wananchi kwenda kuchukua Vitambulisho hivyo katika Wilaya, Kata na Vijiji vilivyopo karibu nao.

Pia soma:
~ Ugawaji wa NIDA wilaya ya Busega unasuasua zaidi ya mwezi. Wanafunzi tunaotegemea namba kuomba mkopo HESLB hatarini kukwama
~ Waziri Masauni: NIDA kuna shida ya usimamizi, Uongozi una shida, Watu wanateseka kupata Vitambulisho
 
Back
Top Bottom