Dankwa Ado Akkufo

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
351
Reaction score
887
MJUE EDWARD AKUFO-ADDO RAIS WA 5 WA GHANA, BABA MZAZI WA NANA DANKWA AKUFO ADDO RAIS WA 12 WA GHANA.

Na.Comred Mbwana Allyamtu
Monday -7/1/2019
Marangu, Kilimanjaro -Tanzania

Edward Akufo-Addo alizaliwa Juni 26,1906 na kufariki Julai 17, 1979, alikuwa ni mwanasiasa, mwanasheria na jaji mkuu wa tatu (3) wa Ghana. Pia alikuwa rais wa tano (5) wa Ghana kwa miaka miwili baada ya kuchaguliwa na wajumbe 164 wa balaza la uchaguzi (164 member of Electoral College) wa bunge la Ghana. Pia ni baba mzazi wa Nana Akufo-Addo, ambae ndie rais wa sasa wa Ghana aliyechaguliwa kuwa rais wa 12 wa Ghana Desemba 7, 2016.

Huyu Edward Akufo-Addo alikuwa ni miongoni mwa wanachama wa awali kabisa na viongozi wa kwanza kuanzisha vuguvugu lilojulikana kama "Big Six" ambalo vuguvugu hili ndilo walio anzisha jukwaa la "Umoja wa Gold Coast" (UGCC), ambapo kupitia umoja huu uliwezesha kupatikana kwa uhuru wa Ghana baadae kwa njia ya amani. Pia Edward Akufo-Addo alikuwa Jaji Mkuu na baadaye Rais wa Jamhuri ya Ghana, tutalitazama hili baadae.

Huyu Akufo-Addo alizaliwa katika mji wa Dodowa chini Ghana. Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi ya kanisa la Presbyterian huko kwenye kitongoji cha Akropong. Kutoka shuleni hapo alifaulu vizuri na mwaka wa 1929, aliingia chuo cha Achimota kusini magharibi mwa Ghana, ambapo Kutoka chuoni hapo alishinda na kupata ufadhiri (scholarship) na kwenda chuo cha St Peter College, Oxford, Uingereza ambako huko alisoma Hisabati, Siasa na Falsafa.

Akufo-Addo baadae aliitwa kwenye Baraza la mafunzo ya sheria (legal council Bar) la London, Uingereza, na mwaka wa 1940 alirudi tena kwa kufanya mafunzo ya sheria kwa vitendo, (law practice) ili kuanza mazoezi ya kisheria mwaka mmoja baadaye.

Baada ya kumaliza mafunzo ya kisheria alilejea Ghana (Gold Coast wakati huo) na mwaka 1947 akawa mmoja ya mwanachama mwanzilishi wa chama cha Umoja wa Gold Coast (UGCC) akiwa na wasomi wengine, vuguvugu lao lilijulikanana kama "Big Six" (siku moja nita andaa makala juu ya waasisi hawa), ambapo ndani ya vuguvugu hilo walikuwepo akina Ebenezer Ako-Adjei, Joseph Boakye Danquah, Kwame Nkrumah, Emmanuel Obetsebi-Lamptey na William Ofori Atta ambao hawa wana julikana kama baba wanzilishi wa taifa la Ghana (founding fathers of Ghana) ambao hawa wote waliwekwa kizuizini na serikali ya kikoloni baada ya kutokea machafuko huko Accra mnamo 1948 kufatia kudai mabadiliko ya katiba.

Kufatia machafuko hayo serikali ya kikoloni ilikubali kufanya mabadiliko madogo kwenye katiba na kuanzia mwaka 1949 hadi 1950, Edward Akufo-Addo alichaguliwa na kuwa mwanachama wa Halmashauri ya mabadiliko ya katiba ya Gold Coast kwenye ile Tume ya Katiba ya Coussey.

Baada ya uhuru wa Ghana Edward Akufo-Addo aliteuliwa kuwa mbunge chini ya serikali ya Kwame Nkrumah na mwaka 1962-64, Akufo-Addo aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Ghana yani mmoja wapo wa Waamuzi watatu waliokuwa wakiendesha kesi kwenye mahakama kuu ya Ghana, laikini baadae alifukuzwa kazi na kuwekwa kizuizini kwa makosa ya Uadilifu na uhaini akiwa pamoja na Tawia Adamafio, Ako Adjei na wengine watatu baada ya kutokea kwa shambulio la bomu kwenye mji wa Kulungugu ambapo shambulio hilo lilimlenga Rais Kwame Nkrumah. Lakini baadae Edward Akufo-Addo aliachiwa huru yeye na wenzake kwa kuondolewa mashtaka pamoja na majaji wenzake kwa kutopatwa na hatia yoyote.

Baada ya mapinduzi ya kuondolewa kwa serikali ya Kwame Nkrumah mwaka 1966, Edward Akufo-Addo aliteuliwa kuwa Jaji mkuu wa Ghana hadi 1970, Edward Akufo-Addo alichaguliwa katika cheo cha Jaji Mkuu na Serikali ya balaza la mapinduzi la Ghana (NLC), na baadae aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba (ambayo tume hiyo iliandaa Katiba ya Jamhuri ya pili ya Jamhuri ya ya Ghana ya 1969). Pia Edward Akufo-Addo alikuwa mkuu wa Tume ya Kisiasa ya NLC wakati huo huo.

Baada ya katiba mpya Edward Akufo-Addo baadae alichaguliwa kuwa rais (Ceremonial president) kuanzia Agosti 31, 1970 hadi alipo achia wadhifa huo kwa hiari yake Januari 13, 1972.Akufo-Addo alikuwa Rais wa Ghana asiye na madaraka makubwa katika Jamhuri ya Pili ya nchi hiyo, huku nguvu halisi ya madaraka ya nchi ilikuwa kwa waziri mkuu, Dk Kofi Abrefa Busia.

Mnamo Julai 17, 1979, saa 11:42 asubuhi Akufo-Addo aliripotiwa kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 73 nyumbani kwake Accra Ghana, kifo chake kilitokana na kifo cha sababu za asili.


Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…