Iweje CCM washinde mijini? jamani tunaamini huku mijini ndiko kuna uelewa mkubwa, magazeti mengi, Redio za kutosha na TV!!!!!!!!
Mijini ndiko kunafukuzwa wamachinga, watu kubomorewa majumba, hebu inakuweje jamani?
Waandishi wote wanaishi mijini.
Wasomi wote wanaishi mijini...................., jamani nielezeni kuna nini? ama CCM huku mjini wanafavya kamchezo gani? ina maana hata wewe uliwachagua ccm 2005?
JF nisaidieni kuna nini basi hatupati kufanya mapinduzi huku mjini na badala yake yake mapinduzi yanafanyika kule Karatu, Tarime,Mpanda na Bariadi?
Jamani kuna nini huku Arusha, Mwanza, Dar na hata hapa Mbeya?
Isayamwita hebu jiulize inakuwaje
Moshi Ndesamburo anawaendesha puta CCM.
Kila kitu ni strategies tu.CHADEMA ilipoamua kujiimarisha Moshi iliona njia pekee ni kuweka mtu ambaye anaweza kukiuza chama kwa wananchi na kupambana na nguvu za CCM.
Jimbo la Moshi ni lulu kwa wapinzani na CCM wanalionea gere sana.Uchaguzi wa 2005 CCM kupitia kwa mlezi wa chama hicho mkoani Kilimanjaro walichangisha zaidi ya miliono 300 za 'kulikomboa' jimbo la Moshi.Wafanyabiashara walitoa mipesa kwa ahadi kedekede za CCM.
Hata hivyo wao CHADEMA walikuwa wameshajiwekea rekodi nzuri ya maendeleo hivyo hawakuwa na kazi kubwa ya kuwapiga kumbo CCM.Kwenye kampeni za Ndesamburo alikuwa anajigamba kutokana na rekodi nzuri ya uwajibikaji kwa wananchi na aliwaambia waziwazi wapiga kura wake kuwa pesa za CCM wazichue na kuzitafuna lakini kura wasiwape.
Kama Moshi wameweza sisi katika miji mingine tunaweza kama tukijipanga kulingana na mazingira husika.Dar es Salaam kwa mfano, wengi wetu ni wakereketwa sana wa mageuzi lakini linapokuja suala la uchaguzi tunawaachia wazee na akina mama.Kada mbalimbali za watu kama makonda, madereva wa daladala, waalimu, wauguzi, wanafunzi, wamachinga na kadhalika ni jeshi kubwa sana kama likiamua kusema hapana kwa njia ya kura.
Haya ndiyo makundi yanayoanzisha maandamano kila mara kudai haki na maisha bora kwa kila mtanzania.Kama makundi haya yakipiga kura na kudhamiria kuing'oa CCM hata kama CCM wakipanga kuiba kura itakuwa ngumu.
Strategies za CCM ni nyingi na kwa kuwa wao ndio walioshikilia dola wanakuwa na uwanja mpana wa kufanya watakalo.Kwa mfano sasa hivi Kikwete ameshaanza kampeni za uchaguzi ujao.Ziara zake mikoani zina lengo la kuweka mambo sawa.Huu ni utaratibu ambao upinzani nao wanatakiwa kuuanzisha.Pale waliposhindwa CCM wao lazima waoneshe wanaweza kwa vitendo.
Jambo jingine ni ubinafsi wa vyama vya upinzani.Linapokuja suala la uchaguzi ni muhimu vyama vikaacha kutugawanya badala yake wakapeana nafasi katika kusimamisha wagombea majimboni.Vyama viachiane majimbo kulingana na nguvu ya chama na mtu husika kusudi upinzani ujipatie wabugne wengi mjengoni.
Mikakati haianzi 2010 ndugu zangu, inaanza leo tena sasa.
Tusiwe mahiri wa kulalamika na kuandamana na kusahau kuwa njia sahihi na nzuri ya kuibana CCM ni sanduku la kura.Hata wakiiba kura hawatadumu milele.
Mungu husikia kilio cha wanyonge na kamwe hataacha mwovu adumu milele. Meseji senti!