IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
Watu wa mijini, mna tatizo gani? ni nani kawaroga? mbona mnaishia maneno bila matendo? iweje huku mjini hamna dhamira ya kweli? iweji watu wasiosoma(hawajaelimika) ndiyo wafanye mageuzi ya kisiasa na ninyi wasomi mnaokaa mijini hamjafanya chochote? maneno tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.............., Mbona hatuna mbuge yoyote toka katika miji hiii niliyoitaja? tunaona watu kule vijijini ndiyo wanaofanya kweli
Hebu inakueje jamani??????????????
Iweje CCM washinde mijini? jamani tunaamini huku mijini ndiko kuna uelewa mkubwa, magazeti mengi, Redio za kutosha na TV!!!!!!!!
Mijini ndiko kunafukuzwa wamachinga, watu kubomorewa majumba, hebu inakuweje jamani?
Waandishi wote wanaishi mijini.
Wasomi wote wanaishi mijini...................., jamani nielezeni kuna nini? ama CCM huku mjini wanafavya kamchezo gani? ina maana hata wewe uliwachagua ccm 2005?
JF nisaidieni kuna nini basi hatupati kufanya mapinduzi huku mjini na badala yake yake mapinduzi yanafanyika kule Karatu, Tarime,Mpanda na Bariadi?
Jamani kuna nini huku Arusha, Mwanza, Dar na hata hapa Mbeya?
Mwita,
Ukitaka kujua ni kwa nini CCM inashinda chaguzi rudi nyuma kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995. Hapa Dar majimbo yote yalichukuliwa na wapinzani hasa NCCR, lakini usalama wa taifa wakafanya vitu vyao, uchaguzi ukarudiwa na ushindi ukaenda CCM. Kule Mbeya mjini Mwaiseje, Katibu Mkuu wa NCCR (kwa sasa) alikuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia chama chake cha NCCR.
Kwa maoni yangu Watanzania wana mwamko wa kisiasa sana. Sehemu kubwa ya matatizo ni CCM. Hawa jamaa, amini usiamini wanaiba kura. Kinachowasaidia sana ni kuwa tume ya uchaguzi inateuliwa na rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, vyombo vyote vya dola vinafanya kazi kufuata matakwa ya CCM, kila wakati Bunge linapovunjwa kuelekea uchaguzi mwingine wabunge wote hupewa milioni 20 (wabunge wengi ni wa CCM na fedha hizo hutumika kugawa takrima). Aidha CCM inatumia fedha za umma kama za BOT kufanyia kampeni. Mbali na haya yote CCM ina mbinu nyingi za kuhujumu uchaguzi. Kumbuka pia semo wa Sumaye, "Mtu akitaka biashara yake ifanikiwe, ajiunge na CCM." Msemo huu si maneno matupu CCM inautumia kwa vitendo. Wafanya biashara na wafanyakazi wasiofanya matakwa ya CCM wanadhibitiwa na serikali ya CCM.
Kwa ujumla, uwanja unaotumiwa wakati wa uchaguzi haujawa tambarare. Hata refa au mwamuzi wa mchezo huwa anatoka upamde wa timu mojawapo ya zinazocheza uwanjani, timu ya CCM. Hata mtandao uliokwisha kujengeka wakati wa chama kimoja kwa kiasi fulani unaisaidia CCM.
Kwa kiasi fulani hii ndiyo hali inayofanya CCM kuendelea kutawala. Siyo kwa sababu watu wanaingu mkono, bali kwa sababu wana mbinu nyingi chafu wanazozitumia kupora kura na kujitangaza washindi.
Isayamwita hebu jiulize inakuwaje Moshi Ndesamburo anawaendesha puta CCM.
Kila kitu ni strategies tu.CHADEMA ilipoamua kujiimarisha Moshi iliona njia pekee ni kuweka mtu ambaye anaweza kukiuza chama kwa wananchi na kupambana na nguvu za CCM.
Jimbo la Moshi ni lulu kwa wapinzani na CCM wanalionea gere sana.Uchaguzi wa 2005 CCM kupitia kwa mlezi wa chama hicho mkoani Kilimanjaro walichangisha zaidi ya miliono 300 za 'kulikomboa' jimbo la Moshi.Wafanyabiashara walitoa mipesa kwa ahadi kedekede za CCM.
Hata hivyo wao CHADEMA walikuwa wameshajiwekea rekodi nzuri ya maendeleo hivyo hawakuwa na kazi kubwa ya kuwapiga kumbo CCM.Kwenye kampeni za Ndesamburo alikuwa anajigamba kutokana na rekodi nzuri ya uwajibikaji kwa wananchi na aliwaambia waziwazi wapiga kura wake kuwa pesa za CCM wazichue na kuzitafuna lakini kura wasiwape.
Kama Moshi wameweza sisi katika miji mingine tunaweza kama tukijipanga kulingana na mazingira husika.Dar es Salaam kwa mfano, wengi wetu ni wakereketwa sana wa mageuzi lakini linapokuja suala la uchaguzi tunawaachia wazee na akina mama.Kada mbalimbali za watu kama makonda, madereva wa daladala, waalimu, wauguzi, wanafunzi, wamachinga na kadhalika ni jeshi kubwa sana kama likiamua kusema hapana kwa njia ya kura.
Haya ndiyo makundi yanayoanzisha maandamano kila mara kudai haki na maisha bora kwa kila mtanzania.Kama makundi haya yakipiga kura na kudhamiria kuing'oa CCM hata kama CCM wakipanga kuiba kura itakuwa ngumu.
Strategies za CCM ni nyingi na kwa kuwa wao ndio walioshikilia dola wanakuwa na uwanja mpana wa kufanya watakalo.Kwa mfano sasa hivi Kikwete ameshaanza kampeni za uchaguzi ujao.Ziara zake mikoani zina lengo la kuweka mambo sawa.Huu ni utaratibu ambao upinzani nao wanatakiwa kuuanzisha.Pale waliposhindwa CCM wao lazima waoneshe wanaweza kwa vitendo.
Jambo jingine ni ubinafsi wa vyama vya upinzani.Linapokuja suala la uchaguzi ni muhimu vyama vikaacha kutugawanya badala yake wakapeana nafasi katika kusimamisha wagombea majimboni.Vyama viachiane majimbo kulingana na nguvu ya chama na mtu husika kusudi upinzani ujipatie wabugne wengi mjengoni.
Mikakati haianzi 2010 ndugu zangu, inaanza leo tena sasa.
Tusiwe mahiri wa kulalamika na kuandamana na kusahau kuwa njia sahihi na nzuri ya kuibana CCM ni sanduku la kura.Hata wakiiba kura hawatadumu milele.
Mungu husikia kilio cha wanyonge na kamwe hataacha mwovu adumu milele. Meseji senti!
Tuliodhani kuwa ni wanamageuzi wametugeuka. Angalia akina Lamwai, Kabourou, Tambwe Hiza,....

Positioning ya yama vya Upinzani katika miji husika ni tatizo kubwa sana... na kama hali itaendelea kuwa katika hali hii basi ni kwamba tutaendelea kuwa Wapinzani tu lakini hatuna meno. Kama tutakuwa tunasubiri Mwaka 2010 ili tuweze enda katika miji husika na kutangaza sera zetu basi ni dhahiri hatutawang'oa CCM.
Vijijini imekuwa ni rahisi kidogo kupambana na CCM kwa kuwa wananchi wa huko are feeling like they are left out and CCM wameweka concerntration kubwa zaidi katika miji mikuu yenye watu wengi. Kwa hiyo nadhani ili kuwang''a CCM inabidi tubadili mwendo na kuwafikia watu zaidi.
Tuliodhani kuwa ni wanamageuzi wametugeuka. Angalia akina Lamwai, Kabourou, Tambwe Hiza,....
Mtu wa Mungu,
Katika uzoefu wangu wa chaguzi barani Africa utaona mijini ndiko mageuzi hufanyika kwa kiasi kikubwa, lakini hapa nyumbani mambo si hivyo, hebu nini kifanyike jamani?