Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ni toka mvua za mwaka jana 2024 mpaka leo barabara za Kichangani kuanzia Shule, Kisimani hadi Msikiti wa Mzee Nandule, kote huko njia hazipo ni kama vile Serikali imesahau kuwa kuna watu wanaishi huko.
Mbali ya kuwa Wananchi wamejichanga na kutafuta vifusi ila mkandarasi wa Barabara ya Kibada - Mwasonga kagoma kutusaidia kifusi cha kuweka hapa ili barabara zipitike.
Tunaiomba Serikali yetu itukumbuke wananchi tumechoka kuchangishwa jamani