#COVID19 Dar: Bila barakoa kwenye Usafiri wa Umma unashushwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imetangaza rasmi kuanza kuwashusha abiria wote ambao wataonekana ndani ya vyombo vya usafiri wa umma bila kuvaa barakoa ikiwa katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Covid-19.

Vyombo vilivyotajwa ni pamoja na daladala, mabasi ya mwendokasi, mabasi yaendayo mikoani, vivuko vya majini ‘pantoni’.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Agosti 12, 2021 katika mdahalo wa kitaifa kuhusu Covid-19 unaoendelea kufanyika hivi sasa katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere JNICC.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija amesema zoezi hilo litafanyika kwa kufanya ukaguzi.

“Abiria ambao watakuwa hawajavaa barakoa tutasimamisha gari na kuwashusha , maagizo yalishatolewa na uelimishaji umefanyika kwa kipindi kirefu kinachotakiwa sasa kila mtu achukue tahadhari".

“Kumekuwa na upotoshaji mwingi katika suala la chanjo na kujikinga lakini tunashukuru mwitikio ni mkubwa, wananchi wameendelea kupokea chanjo imeleta fursa tuna vituo vingi vya kutosha kwenye hospitali zetu waepukane na upotoshaji unaofanyika...

“Afya ni yako mwenyewe, heri kinga kuliko tiba watu wamepata changamoto hizi na zinapojitokeza zinazuia uzalishaji mali,” amesema Makalla.

Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Dk Ntuli Kapologwe amesema mapambano yaliyopo sasa nchini ni namna ya kupambana na upotoshaji wa taarifa za chanjo ya ugonjwa huo.

“Mapambano tuliyonayo sasa ni dhidi ya upotoshaji katika ugonjwa huu, lakini lazima tuangalie chanjo pekee haitoshelezi lazima tujikinge kwa kunawa, kutakasa mikono na kunawa kwa maji tiririka na sabuni lakini pia tukikaa umbali wa mita moja,” amesema.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Dk Fatma Mrisho amesema ni wakati sasa kila mmoja kuhakikisha anaungana na nguvu za viongozi kukinga na kutokomeza ugonjwa huo kwa kufuata kanuni za afya na kuchanja.

Mwananchi
 
Hizi story, maagizo na maelekezo tushayazoea kila uchao kama wameshindwa ku make distance kwenye swala la machinga mf brbr ya uhuru yenye msongamano wa wanafunzi na machinga leo wanakuja na usafiri wa umma wakati hilo tuu limewashinda duuh kweli yetu macho tusikilize viongozi wetu!
 
Huyu mkuu mkoa umemshinda matamko mengi sana na hamna hata moja watu wanatekeleza yani hawajaanza kusema leo lakini wapi watu hawavai.
Angekua bedui Makonda hapa kitambo sana wote level siti na barakoa juu
 
Level seat hawataki kisa watapata hasara mabus/daladala zao.Nn maana ya barakoa wakati watu wanapumuliana usoni mpaka wanakosa hewa,full kugusana afu tunasema tahadhari.
Wekeni level seat ndo njia nyepesi ktk daladala
 
Mafala nyie mnaokazana na mabarakoa
Hizo tutakuwa tunatembea nazo mfukoni mkisimamisha kutukagua tunavaa fasta.Nunueni mabasi yenu ya umma ndo mlete masharti yenu, hata hayo mabasi ya UDA mkikazana na masharti hatupandi, tutanunua hata baiskeli ili zitusaidie kwenye usafiri.
Au wekeni Polisi ndani ya magari ya UDArt nae avae barakoa muda wote asimamie masharti yenu.
Ndo maana mabosi wengi wanakufa kwa kuvaa barakoa muda wote
 
Gaweni bure hizo barakoa, muone watu watavaa au hawatavaa
 
kwanini wasiende na sokoni mteja akija bila barakoa asinunue kitu muuzaji kama hana barakoa afunge genge
 
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imetangaza rasmi kuanza kuwashusha abiria wote ambao wataonekana ndani ya vyombo vya usafiri wa umma bila kuvaa barakoa ikiwa katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Covid-19.

Vyombo vilivyotajwa ni pamoja na daladala, mabasi ya mwendokasi, mabasi yaendayo mikoani, vivuko vya majini ‘pantoni’.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Agosti 12, 2021 katika mdahalo wa kitaifa kuhusu Covid-19 unaoendelea kufanyika hivi sasa katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere JNICC.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija amesema zoezi hilo litafanyika kwa kufanya ukaguzi.

“Abiria ambao watakuwa hawajavaa barakoa tutasimamisha gari na kuwashusha , maagizo yalishatolewa na uelimishaji umefanyika kwa kipindi kirefu kinachotakiwa sasa kila mtu achukue tahadhari".

“Kumekuwa na upotoshaji mwingi katika suala la chanjo na kujikinga lakini tunashukuru mwitikio ni mkubwa, wananchi wameendelea kupokea chanjo imeleta fursa tuna vituo vingi vya kutosha kwenye hospitali zetu waepukane na upotoshaji unaofanyika...

“Afya ni yako mwenyewe, heri kinga kuliko tiba watu wamepata changamoto hizi na zinapojitokeza zinazuia uzalishaji mali,” amesema Makalla.

Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Dk Ntuli Kapologwe amesema mapambano yaliyopo sasa nchini ni namna ya kupambana na upotoshaji wa taarifa za chanjo ya ugonjwa huo.

“Mapambano tuliyonayo sasa ni dhidi ya upotoshaji katika ugonjwa huu, lakini lazima tuangalie chanjo pekee haitoshelezi lazima tujikinge kwa kunawa, kutakasa mikono na kunawa kwa maji tiririka na sabuni lakini pia tukikaa umbali wa mita moja,” amesema.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Dk Fatma Mrisho amesema ni wakati sasa kila mmoja kuhakikisha anaungana na nguvu za viongozi kukinga na kutokomeza ugonjwa huo kwa kufuata kanuni za afya na kuchanja.

Mwananchi
Hayo maneno tuu walisema level city mi kila siku natoka posta ni nyomi hadi pa kupumulia hakuna
 
Barakoa zinasaidia sana Mkuu wa Mkoa anahitaji uungwaji mkono.
 
Kuvaa barakoa ni hatari kuliko kutokuvaa barakoa maana ile shika vitu vingine njiani na kisha kupeleka mkono mdomoni au karibu na mdomo kurekesbisha barakoa ikiwa pamoja na kuvua ni kumsogeza adui chumbani.
 
Back
Top Bottom