Dar: CCM yatembelea daraja la Bilioni 24 Bonyokwa

Acha tupigwe
 
ccm huwa wanakula kuanzia ngazi ya kata, huko kata wameachiwa madiwani,wabunge ,wakaurugenzi wa wilaya, halafu kule juu wanakubali wenyewe
Hii nchi hatari sana.

Ukiifikiria na ukifikiria aina ya viongozi tulio nao unaona kabisa tuna safari ndefu sana kufikia maendeleo ya kueleweka.

Kwa kifupi wizi ndio kipaumbele cha kwanza kwa kila mfanyakazi wa serikali wa hii nchi.

Kibaya zaidi ufuatiliaji wa matumizi ya mapato yetu ni kama wafu wasiotambua lolote.

Unaletewa boti la m70 unaambiwa b1.5 unakubali tu.

Unaletewa coaster ya m100 au pungufu unaambiwa ya m325 unakubali tu.

Ujakaa sawa unaletewa kidaraja uchwara ambacho hakivuki b10 unaambiwa b24 unakubali tu.

Tuna safari ndefu sana.
 
na uzuri wanajua namna ya kula na kugawana, na ndio maana CAG anaongea yanaisha
 
Mleta Uzi kishakula zake elfu 7 hana wasiwas,anatuchora tu tunaojifanya tuna uchungu na nchi 😁😁😁
 
Shilole yupo EDA anakata vitunguu huku nchi inapigwa
Hata asingekuwa eda hakuna cha maana ambacho angefanya.

Au we unadhani kuna kipi cha maana angefanya kuzuia upigaji?

Mtu anayesema hadharani;

"Kuleni kwa urefu wa kamba zenu msiingiliane"

"Wasome wezi hadharani wasikie majina yao waone aibu"

"Nyie wakuu wa mikoa nawahamisha ili kuwalinda na makosa yenu"

Utarajie nini cha maana kutoka kwa mtu huyo?

Kwa kifupi nchi inanyambuliwa na kuliwa kwa viwango vya juu kuliko wakati wowote ule.

Tena watu wanafidia walipopoteza wakati wa magu na wanaweka akiba ya kutosha kwa ajili ya rais ajaye kwani anaweza akawa na tabia za magu wakapoteza tena.

Kwahiyo watu wanainyambua nchi vilivyo.

Ni hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…