LGE2024 Dar: CHADEMA wasusia uchaguzi Temeke, wawaondoa mawakala wao vituoni

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Wakuu,

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke, Dar es Salaam kimetangaza kususia uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 unaoendelea sasa, kutokana na kile walichodai kuwa fomu za mawakala wao zimebadilishwa vituo hatua iliyopelekea mawakala hao kushindwa kuingia kwenye vyumba vya kupigia kura ili kutimiza majukumu yao kama kanuni inavyoelekeza

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Temeke Benitho Mapinga amesema wameususia uchaguzi katika wilaya hiyo kutokana na sintofahamu zinazoendelea kwenye maeneo mengi ikiwemo katika mtaa wa Keko Machungwa, ambako amedai kuwa viapo vyote vya mawakala wa CHADEMA eneo hilo vimechezewa ambapo wamebadilishiwa vituo vya kusimamia uchaguzi sambamba na kuwacheleweshea kuwapa viapo vyao kwani wamewapatia viapo hivyo wakati ambao zoezi hilo limeshaanza

"Wamefanya haya yote wakitambua wazi kabisa kuwa wakala ni mali ya chama wanambadilishiaje direction wao?, wakala hausiki na Tume (TAMISEMI) tunamlipa sisi kwa kila kitu, tumemgharamia sisi kufika popote pale lakini wao wameamua, kwa hiyo msimamo wetu na msimamo wangu kama Mwenyekiti wa wilaya hii nimeamuru mawakala wote wa wilaya hii waondoke kwenye vituo vya uchaguzi" -Mapinga

Kwa upande wake, Michael Peter Mbuya ambaye ni Mjumbe wa CHADEMA wilaya ya Temeke amesema yeye ndio kiongozi wa chama aliyehusika kwenda kuchukua viapo na kuwatambulisha mawakala wao

"Saa 01:55 asubuhi niliwapeleka mawakala wangu katika vituo vyote vya mtaa wetu wa Keko Machungwa ambapo vituo vilikuwa 28, yaani serikali ya mtaa vilikuwepo nane, Barabara ya Mkenga vinne, Shule ya Msingi Baraksi 16, baada ya kufika kwenye shule ya msingi Baraksi tukaambiwa tutoe viapo, nikampigia Mtendaji wa Kata yeye akasema ameshamkabidhi Mtendaji wa mtaa, Mtendaji wa mtaa ambaye anaitwa Sarah Saidi, baada ya kufika kwa Mtendaji wa mtaa akatuzungusha mpaka kufika saa 02:00 asubuhi tukamwambia muda unaenda tupe viapo, yeye akaita Polisi akasema tunamfanyia vurugu" -Mbuya

Mbuya ameendelea kufafanua kuwa baada ya Polisi kufika wakamwabia Mtendaji akabidhi viapo, ndipo Mtendaji akawakabidhi viapo viongozi wa CHADEMA ambao nao Walienda kuwakabidhi moja kwa moja mawakala wao na hapo ndipo waliposhangazwa kuona vituo walivyowapangangia mawakala wao vimebadilishwa
 
Kwa nini mawakala wa CCM fomu zao hazinaga utata?

Nchi hii ipo chini ya dikteta
 
Wakuu,

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke, Dar es Salaam kimetangaza kususia uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 unaoendelea sasa, kutokana na kile walichodai kuwa fomu za mawakala wao zimebadilishwa vituo hatua iliyopelekea mawakala hao kushindwa kuingia kwenye vyumba vya kupigia kura ili kutimiza majukumu yao kama kanuni inavyoelekeza​

Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Temeke Benitho Mapinga amesema wameususia uchaguzi katika wilaya hiyo kutokana na sintofahamu zinazoendelea kwenye maeneo mengi ikiwemo katika mtaa wa Keko Machungwa, ambako amedai kuwa viapo vyote vya mawakala wa CHADEMA eneo hilo vimechezewa ambapo wamebadilishiwa vituo vya kusimamia uchaguzi sambamba na kuwacheleweshea kuwapa viapo vyao kwani wamewapatia viapo hivyo wakati ambao zoezi hilo limeshaanza​

"Wamefanya haya yote wakitambua wazi kabisa kuwa wakala ni mali ya chama wanambadilishiaje direction wao?, wakala hausiki na Tume (TAMISEMI) tunamlipa sisi kwa kila kitu, tumemgharamia sisi kufika popote pale lakini wao wameamua, kwa hiyo msimamo wetu na msimamo wangu kama Mwenyekiti wa wilaya hii nimeamuru mawakala wote wa wilaya hii waondoke kwenye vituo vya uchaguzi" -Mapinga​

Kwa upande wake, Michael Peter Mbuya ambaye ni Mjumbe wa CHADEMA wilaya ya Temeke amesema yeye ndio kiongozi wa chama aliyehusika kwenda kuchukua viapo na kuwatambulisha mawakala wao​

"Saa 01:55 asubuhi niliwapeleka mawakala wangu katika vituo vyote vya mtaa wetu wa Keko Machungwa ambapo vituo vilikuwa 28, yaani serikali ya mtaa vilikuwepo nane, Barabara ya Mkenga vinne, Shule ya Msingi Baraksi 16, baada ya kufika kwenye shule ya msingi Baraksi tukaambiwa tutoe viapo, nikampigia Mtendaji wa Kata yeye akasema ameshamkabidhi Mtendaji wa mtaa, Mtendaji wa mtaa ambaye anaitwa Sarah Saidi, baada ya kufika kwa Mtendaji wa mtaa akatuzungusha mpaka kufika saa 02:00 asubuhi tukamwambia muda unaenda tupe viapo, yeye akaita Polisi akasema tunamfanyia vurugu" -Mbuya​

Mbuya ameendelea kufafanua kuwa baada ya Polisi kufika wakamwabia Mtendaji akabidhi viapo, ndipo Mtendaji akawakabidhi viapo viongozi wa CHADEMA ambao nao Walienda kuwakabidhi moja kwa moja mawakala wao na hapo ndipo waliposhangazwa kuona vituo wali​

yote hayo tuliyategemea ccm ni laana kwa taifa
 
Yani ukidharau nafasi ya
Mwenyekiti
Mjumbe
Wenzako mpaka uhai wanatoana kisa tu kuwa Mwenyekiti au Mjumbe
 
CCM mnatia aibu. Halafu mkikaa wenywe mnajidanganya mnapendwa. Toeni haki
 
Back
Top Bottom