Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Picha hii kwangu inanikumbusha miaka yangu ya mwanzo udogoni naanza kujitambua na kuingia kwenye duka la vitabu kununua vitabu.
Nimenunua vitabu vingi duka hili kuanzia mwaka wa 1963 nikiwa na umri wa miaka 11.
Safari ya kutoka nyumbani kuja "Picha ya Bismini," (Askari Monument) ilikuwa safari makhsusi.
Nitaoga na kuvaa, "Sunday Best," nguo zangu nzuri nizipendazo.
Kwa miaka ile Dar es Salaam Bookshop ilikuwa ikiongoza kama duka bora la vitabu mji mzima.
Nilikuwa nikiingia ndani ya duka hili nilikuwa naingia katika dunia ambayo mimi peke yangu nilikuwa naielewa.
Nakuwa sipo Dar es Salaam niko angani na hakuna viumbe vingine ila mimi na vitabu.
Nitatembea ndani mle kutoka shubaka moja hadi lingine, shubaka lingine hadi lile na lile hadi lingine.
Nachukua kitabu kimoja natazama picha kwenye cover na jina la kitabu, "Adili na Nduguze," Shaaban Robert, "Machimbo ya Mfalme Suleiman," Rider Haggard, Alif Lela Ulela orodha ndefu.
Itachukua muda kuamua ninunue kitabu kipi.
Nikitoka kwenye vitabu naingia kwenye sehemu ya zana za uchoraji kwani nilikuwa artist.
Water colours gani zimeingia na brush zipi.
Penseli za Staedtler na vifutio vyake.
Siku zile zilikuwa siku za neema kila ukiingia Dar-es-Salaam Bookshop wana vitabu vipya haba jana.
Namkumbuka dada mmoja alikuwa pale counter.
Baada ya miaka mingi dada huyu nikaja kumuona sasa si msichana tena ni mama mke wa marehemu Mbaruku Mwandoro na mimi si mvulana mdogo ni kijana mkubwa.
Hakuna kitu kilichokuwa kinanipa furaha kama kuweka vitu vyangu kwenye kaunta nikalipa kisha nikafungiwa na kutiliwa kwenye mfuko nadhifu wa kuvutia.
Miaka mingi sana ikapita.
Iko siku nimepita Dar-es-Salaam Bookshop ikanijia hamu na fikra niingie ndani.
Sikustahamili.
Nilitoka nje haraka.
Ningelia wapita njia wenzangu wasingeniacha wangenikimbiza haraka hospitali.
Labda kachanganyikiwa ghafla.
Msongo wa mawazo.
Sijapata ujasiri wa kurejea mahali pale tena.
Nikawa najiuliza nini kimeisibu nchi yangu?