TRA Tanzania
Senior Member
- Jul 16, 2022
- 128
- 370
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema mwezi huuu wa Disemba ni mwezi wa kuwashukuru na kuwasikiliza walipakodi wote nchini.
hayo yamebainishwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Yusuph Juma Mwenda leo tarehe 11/12/2024 ofisini kwake jijini Dar es Salaam alipokutana na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) kwa lengo la kuwasikiliza na kuwashukuru kwa kuendelea kulipa kodi na kuwezesha walipokodi wengine kufanyabiashara.
Aidha, Kamishna Mkuu amesema yeye pamoja na menejimenti ya TRA hawatakaa ofisini mwezi huu bali watatoka kwenda kuwafuata na kuwasikiliza walipakodi.
" Desemba ni mwezi wa kuwashukuru walipakodi wote nchini ...lakini huuu mwezi wa kusikiliza walipakodi wote Tanzania... tumeambizana Makamishna wote, wakurugenzi wote, mameneja wote hawatakaa ofisni bali wataenda kuwasikiliza walipakodi"
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania, Bw. Geofrey Mchangila ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Citibank ameshukuru kukutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu na wameweza kujadiliana mambo mbalimbali ambayo yataendelea kuboresha sekta ya fedha na kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Naye Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna amesema TBA itaendelea kushirikiana na TRA kuhakikisha kwamba mabenki yataendelea kulipakodi sahihi na kwa wakati kwa manufaa ya nchi.