Hatari tuliyokuwa nayo katika jiji la Dar hasa sehemu za Kariakoo ni ujenzi wa maghorofa usiozingatia sio viwango tu bali hata kanuni na taratibu za ujenzi kama zilivyowekwa na jiji!! Hivi sas kuna maghaorofa pale Kariakoo, hasa yale yaliyojengwa na wajenzi wakichina yamekwishaanza kupata nyufa na hayajamaliza hata mwaka!! Ninawasiwasi juu ya miundombinu ya maji taka hasa sehemu za Kariakoo kama itahimili kubeba uchafu utakaokuwa unatoka kwenye hayo maghorofa yanayoporomoshwa kama uyoga.