Pre GE2025 Dar es Salaam: CV za Wabunge mwaka 2020 - 2025. Mbunge wako ametimiza ahadi zake?

Pre GE2025 Dar es Salaam: CV za Wabunge mwaka 2020 - 2025. Mbunge wako ametimiza ahadi zake?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakuu,

Wabunge wa Dar es Salaam: Elimu, Safari za Kisiasa, na Majukumu

1. Jerry Slaa - Mbunge wa Ukonga

Chama: CCM
Uchaguzi wa 2020: Kura 120,936 dhidi ya Asia Daudi Msangi (CHADEMA) aliyepata kura 21,634.

Elimu:

Shule ya Msingi Ukonga
Sekondari ya Pugu na Jitegemee (Advance Level)
Shahada ya Elektroniki na Mawasiliano (2002-2005, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam)
Cheti cha Uhasibu (NBAA, 2002)
Masters of Business Administration (2011-2015, Estami au Maastrich).

Safari ya Kisiasa:

Diwani wa Ilala (2005-2015)
Meya wa Ilala (2010-2015)
Mwanachama wa Kamati Kuu ya CCM (2012-2017)
Mbunge tangu 2020
Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (2022-2023).

2. Kitila Alexander Mkumbo - Mbunge wa Ubungo

Chama: CCM
Uchaguzi wa 2020: Kura 63,221 dhidi ya Boniface Jacob (CHADEMA) aliyepata kura 20,620.

Elimu:

Shule ya Msingi Mgela
Sekondari ya Mwenge na Pugu
Bachelor of Science (Ed), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1997-1999)
Masters in Social Psychology (2000-2002)
PhD in Social Psychology (2003-2008, Southampton, UK).

Safari ya Kisiasa:

Katibu Mkuu Wizara ya Maji (2017-2020)
Waziri wa Uwekezaji na Viwanda (2020-2023)
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji.

3. Dorothy George Kilave - Mbunge wa Temeke

Chama: CCM

Uchaguzi wa 2020: Kura 192,756 dhidi ya Yahaya Omary (ACT-Wazalendo) aliyepata kura 13,263.

Elimu:

Shule ya Msingi Kifungilo
Sekondari ya Jangwani
Mafunzo kutoka Tengeru na Aga Khan Institute.

Safari ya Kisiasa:

Mwenyekiti wa UWT Kata (2008-2011)
Diwani wa Viti Maalum (2011-2015)
Mwenyekiti wa UWT Kanda (2017).

Majukumu Bungeni: Michango 14 na maswali 68 hadi Oktoba 2024.

4. Bonnah Ladislaus Kamoli - Mbunge wa Segerea

Chama: CCM

Uchaguzi wa 2020: Kura 76,828 dhidi ya Edward John Mrema (CHADEMA) aliyepata kura 27,612.

Elimu:

Shule ya Msingi Kalangalala
Bachelor in Computer Science (Learn IT, 2008-2012)
Postgraduate Diploma in International Relations (2014-2015).

Safari ya Kisiasa:

Diwani wa Kipawa (2010-2015)
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya (2012-2017)
Mjumbe wa Kamati ya Masuala ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Majukumu Nje ya Siasa:

CEO wa For You Classic Boutique
Mkurugenzi wa S & B Marketing Consultants.

5. Mussa Azzan Zungu - Mbunge wa Ilala

Chama: CCM

Uchaguzi wa 2005: Mbunge wa Ilala tangu 2005.

Elimu:

Shule ya St. Joseph’s (Forodhani)
Stashahada ya Ufundi wa Anga na Urubani, Kanada.

Safari ya Kisiasa:

Diwani wa Kata ya Mchikichini (2000-2005)
Naibu Meya wa Ilala (2003)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (2020).

6. Jafari Abdallah Chaurembo - Mbunge wa Mbagala

Chama: CCM

Uchaguzi wa 2020: Kura 280,003 dhidi ya Khadija Mwago (ACT-Wazalendo) aliyepata kura 13,985.

Elimu:

Shule ya Msingi Mabibo
FTC in Civil Engineering (DIT, 2004-2006).

Safari ya Kisiasa:

Diwani wa Charambe (2010-2020)
Meya wa Temeke (2015-2020).

Majukumu Nje ya Siasa: Engineer wa DAWASCO (2007-2015).

7. Tarimba Gulam Abbas - Mbunge wa Kinondoni

Chama: CCM

Uchaguzi wa 2020: Kura 112,014 dhidi ya Susan Anselmi Lyimo (CHADEMA) aliyepata kura 11,260.

Elimu:

Diploma in Journalism (TSJ, 1981)
Diploma in Gaming and Slots (Uholanzi, 2007)
Certificate in Laws (UDSM, 2010)
Master’s degree in law (UDSM, 2011).

Safari ya Kisiasa:

Diwani wa Kinondoni
Mkurugenzi wa Bahati Nasibu ya Taifa (1975-2003).

Majukumu Nje ya Siasa:

Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania (2017).

8. Issa Jumanne Mtemvu - Mbunge wa Kibamba

Chama: CCM

Uchaguzi wa 2020: Kura 54,496 dhidi ya Stanley Ernest Mgawe (CHADEMA) aliyepata kura 19,744.

Elimu:

Shule ya Msingi Muhimbili (1986-1992).

Safari ya Kisiasa:

Diwani wa Kata ya Kibamba.

Majukumu Bungeni: Mjumbe wa Kamati ya Bajeti (2021-2023).
 
Wale wa Birmingham tujuane tujipige kifua tukisubiria zile Boti toka Japan zije
 
Back
Top Bottom