KERO Dar es Salaam: Kituo cha Mafuta Oasis - Mwenge kimegeuka kuwa kituo cha daladala na bajaj

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kituo cha Mafuta cha Oasis kilichopo Mwenge kimegeuka Kituo cha Daladala na Bajaj kiasi cha kuhatarisha maisha na kuwa kero kwa watumiaji sahihi wa kituo hicho.

Mamlaka husika shughulikieni hili kabla majanga hayajajitokeza, kwani sehemu moja iwe kituo cha vyombo vyote hivyo huku vingine vikiingia na kutoka muda wote huku pia mpishano wa watu ukiwa wa kiwango cha juu hasa jioni, siku kukitokea tatizo waathirika wanaweza kuwa wengi.




 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…