TRA Tanzania
Senior Member
- Jul 16, 2022
- 128
- 370
Leo tarehe 22.11.2024 Chuo cha Kodi (ITA) kimefanya mahafali ya 17 ya chuo hicho. Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya ambaye amewataka wahitimu kuwa mabalozi wazuri wa chuo hicho na kuwa vinara katika kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari pamoja na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.