Dar es Salaam: Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Buza ahukumiwa kwenda jela miaka 2

Dar es Salaam: Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Buza ahukumiwa kwenda jela miaka 2

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
1680694686775.png
Kama tunavyoelezana kila siku kuwa hakuna aliye juu ya Sheria. Mkionewa muwe mnachukua hatua bila kutizama sura ya mtu. Yeyote anaweza kushitakiwa, akakutwa na hatia na akatumikia adhabu.

Tarehe 4/4/2023, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, Mheshimiwa JOHN MASHAURI NGEKA amemhukumu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sigara Buza Temeke Philemoni Shabaha Gotta kwenda jela miaka miwili na kulipa fidia ya Tshs 1,300,00/=.

Mwenyekiti alituhumiwa kwa kumpiga na kumjeruhi Samwel Mpoi aliyefika ofisini kwa mwenyekiti huyo kudai mali zake Subwoofer na Tv vilivyozuiliwa hapo kama dhamana ya malipo ya Tshs 900,000/=.

Kupiga ni kosa na kujeruhi ni kosa.
 
Kama tunavyoelezana kila siku kuwa hakuna aliye juu ya Sheria. Mkionewa muwe mnachukua hatua bila kutizama sura ya mtu. Yeyote anaweza kushitakiwa, akakutwa na hatia na akatumikia adhabu...
Takataka za Magufuli hizo... bahati haikua upande wake maana Fashisti angekua hai angemzawadia ukuu wa mkoa!!
 
Sheria zetu haziko sawa,

Kupiga na kujeruhi,
jela miaka 2 na faini juu

Ufisadi wa mabilioni,
Kifungo Cha nje na faini kiduchu

Sijui alieturoga nani[emoji3525]

Sent using JamiiForums mobile app
 
Hiyo pesa uliyoandika ni shingapi.?

Kama hamuwezi kuandika muombage msaada..

All in all baada ya kulipwa hiyo je atalipwa na hivyo vitu vyake vilivyouzwa.??
 
Namfahamu Sana Bwana Gotta Mwanajeshi mstaafu,huyu jamaa tangu alipoingia tu pale Sigara ofisi ikamshinda ila ni vile nchi hii imejaa watu wa hovyo tu.

Gotta ni tofauti sana na mtangulizi wake Bwana Ngonyani aliyeiongoza Sigara vyema kwa miongo miwili karibia,Jiwe alituwekea Watu wa hovyo sana kwenye nafasi za muhimu.

Sent from my Nokia 1.4 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom