Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, wananchi wamehimizwa kushiriki kikamilifu katika kampeni za wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.
Wito huo umetolewa na Afisa Uchaguzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Maduhu William, katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Jijini Dar es Salaam.
Wakili Maduhu aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuwasikiliza wagombea na kuwachagua viongozi watakaoleta ufumbuzi wa changamoto zao.
Soma pia: LHRC: Sheria Mpya za Uchaguzi zimeacha maoni ya Wadau kuhusu maamuzi ya Tume ya Uchaguzi kuhojiwa Mahakamani
Anna Sangai kutoka idara ya Mafunzo na Ujenzi wa Nguvu kwa Pamoja TGNP, alibainisha kuwa mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa wa wananchi juu ya masuala ya uchaguzi na kuangazia vikwazo wanavyokumbana navyo wanawake katika kugombea nafasi za uongozi.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, akiwemo Tatu Ally, walitoa pongezi kwa TGNP kwa kuandaa mafunzo haya ya kutoa elimu juu ya uchaguzi na uongozi.
Walisema kuwa bado kuna changamoto kubwa kwa wanawake wanaotamani kushiriki nafasi za uongozi.
Mafunzo hayo, yaliyofanyika kwa kushirikisha wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam, yaliangazia pia mada ya "Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Je, Wananchi Wanajua Kanuni na Taratibu za Uchaguzi?"
Source: Safari Media