TRA Tanzania
Senior Member
- Jul 16, 2022
- 128
- 370
Dar es Salaam, 01 Januari, 2025:
Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inautaarifu umma kuwa, katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/25 (Oktoba – Desemba 2024) imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 8.741, sawa na ufanisi wa asilimia 104.63 ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 8.354, na ukuaji wa asilimia 19.05 ukilinganisha na kiasi cha Shilingi Trilioni 7.342 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2023/24.
Aidha, katika robo ya pili ya mwaka 2024/25, Mamlaka ya Mapato Tanzania imevunja rekodi ya makusanyo kwa mwezi wa Desemba, 2024, kwaweza kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 3.587, ambacho ni kiwango cha juu kabisa kukusanywa kwa mwezi mmoja toka kuanzishwa kwa TRA, na hivyo kuvunja rekodi iliyokuwa imewekwa mwezi Desemba 2023 ya kukusanya Shilingi Trilioni 3.050.
Katika mwezi Desemba 2024, Mamlaka ya Mapato Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 3.587, sawa na ufanisi wa asilimia 103.52 ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 3.465, na ukuaji wa asilimia 17.59 ukilinganisha na kiasi cha Shilingi Trilioni 3.050 zilizokusanywa mwezi Desemba 2023, kama inavyoonekana katika Jedwali Na. 1.