Dar es Salaam: Uzuri uliojificha vol.2

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
Dar es Salaam Dar es Salaam Dar es Salaam, Jiji la pili kwa ukubwa Afrika Mashariki. Limetajwa katika tungo za nyimbo kibao na wasanii wa kila kizazi.Jiji lenye mjumuiko wa makabila yote 126 napa nchini na watu wa mataifa mbalimbali.
Lakini limekuwa likijulikana kama Jiji la kibiashara zaidi ,Jiji la kusaka pesa,Kanakwamba Mazuri mengi ya jiji yamewekwa mfuko wa Nyuma.
Uzi huu ni muendelezo wa Makala maalum zenye kukujuza juu ya mazuri ya Jiji hili

Kwa wote wenye kupenda kutalii na kufurahia Uzuri wa asili na kujengwa katika mandhari ya Miji na Majiji...msiende mbali, msiumize kichwa kwani "Dar es Salaam" imesheeni sehemu lukuki ambazo zitakupa tabasamu.

Kuna sehemu kibao ambazo inawezekana ulikuwa haujui,ila kupitia nyuzi hii,nimetazamia kukujulisha...

Katika Volume ya Pili ya Makala ya DAR ES SALAAM : UZURI ULIOJIFICHA, tutaangazia zaidi maeneo na vivutio vilivyo ndani ya Wilaya ya Ubungo,Temeke na Kigamboni.
Karibuni Dar es salaam
 
Sasa mbona haujataja hivyo vivutio hata kimoja mkuu 😎
 
tutaangazia zaidi maeneo na vivutio vilivyo nje ya Wilaya ya Ubungo,Temeke na Kigamboni.
Karibuni Dar es salaam

Vivutio vilivyo NJE ya wilaya ya ubungo,Temeke na Kigamboni

Kwa hiyo tunaongelea Kinondoni na Ilala
 
KISIWA CHA SINDA:I
Kata : Kibada
Wilaya : Kigamboni
Historia : Ni moja kati ya visiwa vinne vilivyopo katika Pwani ya Kusini mwa Dar es Salaam.Kilifikiwa kwa mara ya kwanza na Ibn Majid mwaka 1470.
Hakuna makazi ya watu kisiwani.
Kisiwa kina
  • Fukwe zenye mchanga mweupe
  • Msitu,Mibuyu ,
  • Ndege na
  • Uoto wa mikoko
  • Mazaria ya samaki na matumbawe
  • Mgahawa
Utafaidi :
  • Kuogelea
  • Canoeing
  • Picnic
  • Utembezi kwenye msitu
  • Kuona ndege
  • Kuona gofu
  • Kula vyakula vya baharini

Mtalii ndani ya Fukwe ya Sinda

Pango ufukweni

Ndege kwenye msitu wa Sinda

Watalii ndani ya Sinda

Gofu katika Kisiwa cha Sinda

Hapa ni Sinda wala si Maldives


Msosi mtamu

Unafikaje :
  • Kutokea Makumbusho Chukua usafiri mpaka Kivukoni,panda pantoni na uvuke ,fika stendi ya feri
  • Kutokea Karume Panda basi ya Kigamboni pitia daraja la Nyerere na ushuke mwisho wa route,ambapo ni stendi ya feri.
  • Panda gari ya Kibada/Cheka ,Ushuke njia ya kwenda kipepeo beach.
  • Hotel ya Kipepeo kuna usafiri wa boti kwenda Sinda
Gharama :
  • Nauli : Daladala ...3,000
  • Boat+Kiingilio+Chakula+Kinywaji....50,000 kwa mtu mmoja
Usalama : 95 %
Mda : saa 4:30 asubuhi - 10:30 jioni.
 
Vivutio vilivyo NJE ya wilaya ya ubungo,Temeke na Kigamboni

Kwa hiyo tunaongelea Kinondoni na Ilala
Samahani,nili azimia kuandika ndani...
Tayari nishafanya marekebisho...
 
Nitaja Tembelea Siku Moja Inshallah Endelea Kumwaga sela Tupate Madini
 
MLIMANI CITY:II
Kata : Ubungo
Wilaya : Ubungo
Historia : Mlimani City ni mjumuiko wa Soko kubwa la bidhaa zilizochakatwa, Kumbi za Mikutano na Makazi.Mlimani City ilizinduliwa mwaka 2006.
Ndani yake kuna
  • Mlimani City Mall: Ambalo ni Soko kubwa la ndani hapa nchini na lenye mfumo wa viyoyozi.
  • Mlimani Conference Cente : Ukumbi mkubwa wa matamasha na mikutano
  • Mlimani Villas : Makazi kupanga
Utafaidi :
  • Maduka ya makubwa ya kimataifa ya vifaa vya Umeme,Electronic na Mawasiliano
  • Maduka makubwa ya mahitaji ya Ndani
  • Migahawa mikubwa ya Chakula na Vinywaji
  • Ukumbi wa kutazama filamu mpya zinazotoka kimataifa
  • Michezo ya watoto
  • Huduma za Kibenki
  • Huduma za makazi
  • Huduma ofisi
  • Huduma za mikutano

Lango kwenda maduka ya Benki

Jengo la Ukumbi

Mojawapo ya maduka

Mgahawa wa chakula wa KFC

Ukumbi wa kuonesha filamu

Ndani ya Ukumbi wa mikutano

Unafikaje : Kutokea Makumbusho/Tegeta /Kawe ,panda gari za kuelekea Simu 2000 shuka Mlimani
Kutokea Gongo la Mboto/Segerea/Mbezi,panda gari za kwenda Makumbusho shukia Mlimani.

Gharama : Nauli....1,500 na hakuna kiingilio

Usalama : 90%
 
Wow!!!
Ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…