Dar es Salaam: Wanigeria wakamatwa wakisafirisha heroin

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
RAIA wawili wa Nigeria, Prince Uche Igwilo(39) mkazi wa Bunju na Hanifa Ally Chig'wele( 22) mkazi wa Tegeta kwa Ndevu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha kilo sita za dawa za kulevya aina ya Heroin.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo Juni 9,2021 na Wakili wa Serikali Yusuph Abood mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Joseph Lwambano imedai, washtakiwa walitenda kosa hilo Mei 22,2021 eneo la Machinjioni Tegeta ndani ya Wilaya ya Kinondoni.

Imedaiwa siku na mahali hapo, washtakiwa walikutwa wakisafirisha kilo 6.10 za dawa za Kulevya aina ya Herione.Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 22, mwaka 2021

Wakati huo huo, Oje Ameji Boniface ambaye ni raia wa Nigeria anayeishi Mbezi Makabe anadaiwa kuwa, Mei 24,2021 katika maeneo ya Mbezi beach, Mbezi Makonde na eneo la Mpakani Ubungo alikutwa akisafirisha gramu 316.4 za dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 22, 2021.
 
Hawa wanaingia Tanzania na kuishi mitaani huko? Wapewe masharti makali kabisa kabisa ya kupewa permit au visa za kuingia na kuishi Tanzania. Kuna wanaoingia kwa gea ya dini nao ni hatari sana kwani wanakuwa na agenda za siri. Si wakuchekea hawa.
 
RAIA wawili wa Nigeria, Prince Uche Igwilo(39) mkazi wa Bunju na Hanifa Ally Chig'wele( 22) mkazi wa Tegeta kwa Ndevu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha kilo sita za dawa za kulevya aina ya Heroin.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo Juni 9,2021 na Wakili wa Serikali Yusuph Abood mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Joseph Lwambano imedai, washtakiwa walitenda kosa hilo Mei 22,2021 eneo la Machinjioni Tegeta ndani ya Wilaya ya Kinondoni.

Imedaiwa siku na mahali hapo, washtakiwa walikutwa wakisafirisha kilo 6.10 za dawa za Kulevya aina ya Herione.Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 22, mwaka 2021

Wakati huo huo, Oje Ameji Boniface ambaye ni raia wa Nigeria anayeishi Mbezi Makabe anadaiwa kuwa, Mei 24,2021 katika maeneo ya Mbezi beach, Mbezi Makonde na eneo la Mpakani Ubungo alikutwa akisafirisha gramu 316.4 za dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 22, 2021.

E0NhMwdXIAAW0HL (1).jpeg
 
Huuu mtandao mbona n mkubwa na
Unaendesha na wakubwa sema ndo hvo
Ukikamatwa ww unajipanga
 
Back
Top Bottom