Dar es Salaam Young Africans SC

Dar es Salaam Young Africans SC

kakuruvi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2009
Posts
770
Reaction score
258
Sina shaka mtakubaliana nami kwamba timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Cameroon ya akina Roger Milla ilikuwa timu bora na yenye mvuto wa kipekee. Akina Omam Biyik, Fede, Mboumboh, Emmanuel Kunde, Makanaky. Si mchezo! Na ndio maana hata gwiji la muziki Kabaselle ya Mpanya jitu la miraba minne Pepe Kalle aliliona hili akatunga wimbo wa Roger Milla.

Hakuishia hapo kwa utambuzi wake pia aliiona timu nyingine machachari na tishio ya Tanzania si nyingine ikiwa imeshawahi kuwa Mabingwa wa Tanzania, Africa Mashariki na Kati. Nisikumalizie uhondo tumsikilize gwiji huyu. Ijumaa njema....bonyeza hapo

''http://www.youtube.com/v/Te1oxYJNjp4''
 
Natafuta sana tape ya huu wimbo lakini sijapata.
 
Hao akina Imoro dah huwa wananiacha hoi sijui nao walisha kufa?
 
Hao akina Imoro dah huwa wananiacha hoi sijui nao walisha kufa?

Vipo hivi ila gwiji linapoondoka wanaathirika wengi Emoro, Jolly baby, Pap Tex, Bileku ya Mpasi, aah!
 
Emoro ndiye aliyatangulia kufa kwa kula cahkula chenye sumu hotelini,ndio maana katika ghani za mwisho za Bileku Mpasi utamsikia akisema (mama nabela,ahi ,mama,empire bakuba) akiwa anakumbushia wakati Emoro akilia kwa maumivu ya tumbo baada ya kula chakula chenye sumu.
 
Na inasikitisha sana,
Lakini Pepe kalle bana alikuwa juu hizi nyimbo zake nzuri sana.
Na hii style ya kuwatumia hawa watu wafupi nimeipenda sana.
 
Emoro ndiye aliyatangulia kufa kwa kula cahkula chenye sumu hotelini,ndio maana katika ghani za mwisho za Bileku Mpasi utamsikia akisema (mama nabela,ahi ,mama,empire bakuba) akiwa anakumbushia wakati Emoro akilia kwa maumivu ya tumbo baada ya kula chakula chenye sumu.

Pengo, nilikuwa sifahamu, oh RIP Emoro.
 
Back
Top Bottom