KERO Dar: Foleni Mbezi Africana mpaka mataa ya Kawe hasa asubuhi ni kero, wanaohusika watafute utatuzi

KERO Dar: Foleni Mbezi Africana mpaka mataa ya Kawe hasa asubuhi ni kero, wanaohusika watafute utatuzi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Siku za hivi karibuni eneo la Mbezi Beach Africana kutokea Tegeta mpaka Mataa ya njia panda ya Kawe kumekuwepo na foleni kubwa ambayo imekuwa kero kwa watumiaji wa 'Bagamoyo Road' hasa wanaoelekea Mjini, kupitia njia ya Mwenge au Kawe.

Watumiaji wa njia hiyo kwa muda wa asubuhi tunajikuta tunatumia zaidi saa nzima kutokea Africana hadi Bondeni, hali hii ni kero sana kwa kuwa inasababisha tunashindwa kufika kwa wakati kwenye majukumu.

Suala hili limekuwa likijitokeza kwa nyakati tofauti hata kabla ya kuanza kwa ujenzi wa njia ga Mwendokasi lakini watumiaji wa njia hiyo tunashindwa kuelewa ni shida ambayo imekuwa ikisababisha kero, jana nilidhani labda kuna msafara wa kiongozi wa ngazi za juu Serikalini kama tulivyozoea lakini haikuwa hivyo.

Tunaomba mamlaka husika hasa Traffic wanaosimamia kipande hicho washughulikie hiyo changamoto maana ni chanzo cha kupoteza muda na kuna wakati inaweza kusababisha wataalamu katika nafasi nyeti na muhimu kushindwa kufika kwenye majukumu kwa wakati hali ambayo inaweza kusababisha madhara mbalimbali.

photo_2024-11-20_11-44-00 (3).jpg

photo_2024-11-20_11-44-00.jpg

photo_2023-09-20_07-36-44.jpg
 
Back
Top Bottom