Dar kwenda Mbeya na passo

Hakikisha kabla haujapanda Mlima Kitonga unapumzisha gari hata Dk 10 ili usije ukapasua radiator,
Mazee habari,nauliza kama naweza kwenda Mbeya toka Dar na ka gari kangu haka kadogo ka toyota Passo nina dharula kidogo,na kwa wazoefu mafuta ya kiasi gani naweza tumia,ka passo kenyewe ni kale kadogo ka pistoni 3....kwa mzoefu naomba anidaidie!
 
Katika siku nimesoma jibu sahihi ktk uendeshaji wa gari ni leo, ubarikiwe sana mkuu. Watu wengi wanajifunza kuendesha gari lakini hawajifunzi gari ni nini na ndio maana ukimuuliza dereva kwanini gari inapata moto mpaka maji kurushwa juu atakwambia hii gari nilia mbiwa nisiinunuwe engine zake sio nzuri, kikubwa wao nikuweka D nakukanyaga mafuta songa mbele.
 
hakikisha macho yako yanaona vzr kutoka iringa mpaka makambako kuna ukungu sana hasa kipindi hiki cha baridi....beba debe mbili kuipa gari uzito kidogo upepo njiani hasa unapokutana na malori...me nilitusua dar to mza na IST nilitoka dsm saa tisa usiku saa nne nipo mwanza ila nipumzika 30min singida na 20min dodoma kwa kuzima gari kabisa
 
Saa nne ya asubuhi?
 
asante mkuu na wewe pia ubarikiwe.

Wengi wanafikiri kuendesha gari ni kuweka gia na kuondoka tu. wanasahau kuwa kuelewa engine inafanya kazi vipi ni muhimu sana tena.
 
Mkuu uko sawa kabisa hii nchi ina watu wajinga sana ,tena wenye mentality za kimasikini kabisa. Utakuta huyu naye eti ni msomi.

Back to the point . Hiyo gari unaenda popote kama barabara ni lami.Mimi nimeendesha gari hiyo kutoka Dar mpaka Mwanza bila hata kupumzika. Hao wanaokuambia sijui Kila baada 120KM upumzishe gari huo ni uswahili tupu wala hawana technical factor.

Mkuu nenda safari yako na ninaamini utafika salama kabisa. Achana na waswahili.
 
Kwa hoja hii na uzi ufungwe...ambaye hajaelewa hatakaa aelewe....gari kama ni nzima unaenda popote..

Mkuu safari njema...
Ukipita pale Iringa usisahau kuniletea dada wa kazi..
 
mkuu juzi nimetoka kagera bukoba mpaka Kilimanjaro moshi lakin nililala arusha yaan passo ni gari moja tamu sana na pia nilikuwa peke yangu tu na speed mwisho 1000
 
mkuu juzi nimetoka kagera bukoba mpaka Kilimanjaro moshi lakin nililala arusha yaan passo ni gari moja tamu sana na pia nilikuwa peke yangu tu na speed mwisho 1000
Wenye prado zao watakuja hapa wakukatalie...
 
Mkuu,
Kwa uzoefu wangu wa Passo Dsm - Mby hadi Ichenjezya kwetu inatoboa kabisa. Shida kidogo ni kupanda mlima Kitonga gari ilikuwa inasinzia sana, so inahitaji kuibembeleza, pale usiwe na haraka panda taratiibuu hadi kwa wachoma mahindi pale juu then fungua.

Mkuu, Kwa ujumla kama walivyo shairi GT wengine before, jiepushe kufanya ligi Vs drivers wenyeharaka zao na magari ya nguvu. Be yourself but determined.

Kuhusu wese, hiyo ndiyo raha ya kipekee kwa gari hiyo. Ukianza na full tank na ili uwe amani na fuel gauge, Unaweza kujazilizia Mkm, Mafinga or Makambako, then upo Mafiat.

SAFARI NJEMA MKUU.!!
 
Kwann usifike, jamaa yangu katoka tanga nayo kaenda njombe baada ya wiki karudi bila shida na alikuwa na family
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…