Dar lilikuwa jiji la fursa

Dar lilikuwa jiji la fursa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kuna binti mmoja kutoka Tanga alipata mchumba, ni kijana anaeishi Dar. Mchumba akimuomba sense likizo mwezini mmoja ili wafahamiane vizuri kabla ya harusi.

Yule binti amefika kwa mchumba aliona fursa ya kupika chapati kwani mtaa ule saa nne asubuhi vitafunwa vinakuwa vimekwisha.

Manjonjo yake alianza kupika chapati za nazi. Alianza na chapati 50. Ananiambia mpaka mwezi unakwisha ilibidi apike 200 kwa siku. 100 asubuhi na 100 jioni.

Juzi nimekutana na yule binti, Ameolewa na sasa ni mama wa watoto wawili. Ananiambia hata chapati 50 haziishi sikuhizi hela mtaani hakuna.
 
Magumashi kafanya yake, Jana nimehangaika kupata chenji ya tsh 10'000/- nataka vocha ya 2'000/- Kila duka hamna change eti hawajauza kabisa na muda huo ilikuwa ni alasiri
 
Magumashi kafanya yake, Jana nimehangaika kupata chenji ya tsh 10'000/- nataka vocha ya 2'000/- Kila duka hamna change eti hawajauza kabisa na muda huo ilikuwa ni alasiri

Duhhh,hii ni mbaya sana
 
Dar bado kuna fursa kibao tatizo wafanyabiashara wetu hawako flexible kusoma soko linaendaje.Kuna biashara kama ya Uji,Juice na Matunda ndio zinatamba kwa sasa
 
Mwenge karibia na msikiti kulikuwa na mama anapika vitumbua alikuwa anauza sana na wateja wake ni wafanyabiashara wa eneo lile.Kuanzia mwaka jana alianza biashara ya kukaanga samaki na mihogo jioni anauza na anapata fedha maradufu ya aliyokuwa anapata kwenye vitumbua na kwa sasa ameajiri watu wengine 3 tofauti na mwanzo ambapo alikuwa peke yake
 
Kila jambo na faida na hasara zake. kweny awamu hii ukiangalia fursa utaziona na zitakulipa. simuungi mkono huyo aliyefanya hali kuwa hivi ila najaribu kuonesha upande wa pili wa shilingi. Usiwe miongoni mwa wanaolalamika ila tengeneza pesa kupitia wanaolalamika.
 
Pesa/hela/mshiko/chapaa inalalamikiwa sana kupotea ghafla mtaani...

Kwa maoni yangu pesa haijapotea, ila watu wanatunza pesa zao hawataki mbwembwe kwa sasa...

Nawaambiaje ngoja karibia na uchanguzi mkuu, utaona...

Cc: mahondaw
 
Na wengi ndo wanazidi kutolewa kwenye ajira kuja mtaani..
cc. Maxcom
 
Back
Top Bottom