Kuna binti mmoja kutoka Tanga alipata mchumba, ni kijana anaeishi Dar. Mchumba akimuomba sense likizo mwezini mmoja ili wafahamiane vizuri kabla ya harusi.
Yule binti amefika kwa mchumba aliona fursa ya kupika chapati kwani mtaa ule saa nne asubuhi vitafunwa vinakuwa vimekwisha.
Manjonjo yake alianza kupika chapati za nazi. Alianza na chapati 50. Ananiambia mpaka mwezi unakwisha ilibidi apike 200 kwa siku. 100 asubuhi na 100 jioni.
Juzi nimekutana na yule binti, Ameolewa na sasa ni mama wa watoto wawili. Ananiambia hata chapati 50 haziishi sikuhizi hela mtaani hakuna.