DAR mkoa bora zaidi wakuishi Tanzania

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,641
Reaction score
11,958
Huu ndio ukweli japo wale wanao jiita wamikoani watapinga na kutoa povu lakutosha kabisa kufilia mitumba walio nunua kwa mafungu siku za minada huko vijijini kwao ili waweze kutazamika angalau wanapoingia jijini.

Kokote duniani unapoitaja tz watu watakimbilia kwanza kuhoji kuhusu dar mana hata kama mikoa mingine haijui lakini dar ataijua tu.

Hapa ni sehemu pekee yenye kila aina ya fursa katika nchi hii.
Ukiwa hapa kama una akili zako timamu huwezi kosa pesa, kwasababu kuna kila njia za kutafutia pesa tofauti na mikoa mingine ambapo njia za kutafuta pesa ni chache.
Kuna baadhi ya mikoa hapa nchini mtu unaweza kumaliza wiki hujaingiza hata sh 5000.
Yote ni kwasababu hakuna njia za utafutaji pesa tofauti na kilimo na ufugaji.
Lakini kwa dar hali ni tofauti hapa hata mpiga debe anapata vijisenti japo wengi wangi hawana mpangilio wa matumizi.
Hasa wale wanaohamia kutoka mikoani ambao huchanganywa na starehe kuliko kuweka malengo.
Ukiwa na akili timamu mafanikio kwa dar yatakujia haraka kuliko sehemu yoyote pale tz.

Ni sehemu ambayo kila aina ya bidhaa hupatikana kwa wepesi sana.
Kuna baadhi ya mikoa hata ukiwa na pesa lakini utakosa baadhi ya bidhaa na hata zikiwepo bado zitakuwa na being ya juu.
Kuna mkoa fulani nilikuta vocha ya 1000 ikiuzwa 1200.

Maisha ya kileo yapo dar, hapa kuna kila technology ambayo ni muhimu kwa maisha ya kisasa tofauti na mikoa mingine.

Hapa mtu unaishi kwa kujiamini na bila kuangalia fulani anaongea nini kazi inakuwa ni kwako kuchanganua lipi ni lipi.

Kwa wale wapenda starehe hapa ndio penyewe, utapata kila aina ya starehe unayo itaka kwa kadri mfuko wako unavyo ruhusu.
Nasema mfuko wako kwasababu hapa hakuna undugu kwenye mambo ya starehe hivyo katika nyanja hii tumia kile ulicho nacho ili kuepusha madhara mengine hasa kwa wageni mlizingatie sana hili.
Kama hujui nini maana yake ni nini basi huwezi elewa namaanisha nini.

Fursa za ajira nyingi zipo hapa, ila ukiwa mvivu wa kufikiri unaweza usiione hata moja lakini wenzako wanakupita kwa kasi wakielekea kwenye mafanikio.

Mwisho niseme karibuni sana dar kwetu.

Pia nitumie nafasi hii kuwakumbusha kuwa adui yako mkubwa unapokanyaga dar ambaye unatakiwa kuwa makini nae ni starehe.
Pia msisahau ninyi wageni wetu ile methali isemayo Jogoo la shamba haliwiki mjini.
Mkija hapa kuweni wapole ujanja wa huko kwenu karambangaze hauwezi kuwasaidia hapa jiji.

Ahsante sana,
Furahia maisha na dar yetu.
 
Uko sahihi..... mimi mwenyewe ndoto zangu ni kuhamishia biashara zangu Dar pale mtaji utakaporuhusu....

Huku mikoani akili zinatanuka kwa mwendo wa kinyonga...

Ndio maana matajiri wengi wa mikoani wakifika Dar wanapotelea kwenye majani....
 
Cha kushangaza maneno hayo huwezi kuyasikia kwa tajiri kama Mengi, Bakhresa, Dewiji au Bill Gate.


Ni masikini tu ndio huwa na Mawazo kama ya mleta mada.....

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Uko sahihi..... mimi mwenyewe ndoto zangu ni kuhamishia biashara zangu Dar pale mtaji utakaporuhusu....

Huku mikoani akili zinatanuka kwa mwendo wa kinyonga...

Ndio maana matajiri wengi wa mikoani wakifika Dar wanapotelea kwenye majani....
Ndio ilivyo mkuu, wengi wanashindwa kuliona hilo ila ukweli ni kwamba katika nchi yetu hii dar ndo mkoa pekee wenye nguvu kubwa ya kibiashara.kwa wale wajanja wa kibiashara wanalielewa hili.

Wasome kle kitabu cha Robert T. Kyosaki.
Financial IQ wataelewa haya na art of business school.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…