Dar: Morocco na Mwenge kujengwa barabara za Juu. RC Chalamila ataka kazi ifanyike Mchana na Usiku

Dar: Morocco na Mwenge kujengwa barabara za Juu. RC Chalamila ataka kazi ifanyike Mchana na Usiku

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amemtaka Mkandarasi anayejenga barabara kutoka Mjini kati Ohio hadi Mwenge na Tegeta, kufanya kazi Usiku na Mchana ili kuhakikisha Ujenzi unakamilika mapema.
IMG-20250115-WA0041.jpg

Ameyasema hayo leo tarehe 15 Januari wakati alipotembelea ujenzi wa barabara ya Mwendo kasi awamu ya nne.

Mkuu wa Mkoa amemhimiza mkandarasi kufanya kazi haraka kipindi hiki ambacho hakuna mvua ili asilete visingizio

"Ni wakati sasa kufanya kazi saa 24. Tuongeze juhudi ili barabara ziweze kuisha. Na inapofika mwezi wa 11 Mheshimiwa rais anapoenda kuomba kura kwa Watanzania, kitu moja wapo cha kuonesha si maneno bali barabara, ni Hospitali, Majengo ya Shule. Hii kichelewesha mnamwambia rais aende kuomba kura bila nyenzo. Kwahiyo kichelewesha zaidi mtakuwa ni miongoni mwa watu mnaohujumu juhudi za kuelekea kupata kura nyingi kwanza kwa chama cha mapinduzi na mbili kwa rais Samia". Amesema Chalamila.
IMG-20250115-WA0021.jpg

Naye Mhandisi Rajab Idd Rajab, Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Mwendo kasi awamu ya nne (BRT 4) kutoka Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), amesema Ujenzi wa barabara hii utaunganishwa na ujenzi wa barabara za Juu (flyovers) maeneo ya Morocco na Mwenge kama ile ya Mfugale. Mradi huu wa Barabara za Juu Mwenye na Morocco utajengwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA).

Hadi sasa Ujezi umefika 22% huku muda ukiwa umefika 77%

"Huu mradi ulianza tarehe 01 Novemba 2023 na ulitarajiwa ukamilike tarehe 30 April 2025. Hadi sasa tumetumia 77% ya muda huku Mradi ukiwa umefika 22%. Sababu kubwa ni miundombinu iliyopo chini ya ardhi ya mabomba ya maji ya DAWASA na cables. Tuna changamoto nyingi itabidi mradi utaongezeka muda kidogo". Amesema Mhandisi Rajab Idd Rajab.

Awamu ya Nne ya mradi inatekelezwa kwa kutumia fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia kupitia mradi wa Dar es Salaam Urbarn Improvement project – DUTP, pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

USANIFU WA MRADI

Usanifu wa Mradi ulifanywa na Kampuni ya M/s KUNHWA Engineering & Consulting Ltd’ na ‘Dongsung Engineering Co. Ltd’ na ‘Seoul Houing & communities Corporation’ zote zikitokea Korea; na zilishirikiana na Kampuni ya ‘Aqgola Engineering & Management Services Ltd ya Tanzania.

Usanifu ulifanywa kwa gharama ya Dola za Marekani 2,013,453 (pamoja VAT). Mkataba huu ulikuwa chini ya usimamizi wa TANROADS na ulitekelezwa kwa kutumia sehemu ya fedha za mkopo toka Benki ya Dunia kupitia mradi wa DUTP. Usanifu wa mradi huo ulikamilika tarehe 01 Machi 2022.


Kazi za ujenzi zimegawanywa katika sehemu (Lots) tatu:

Lot 1: Kutoka Katikati ya Mji (CBD) mpaka Mwenge kupitia Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Barabara ya Bagamoyo, Pamoja na kutoka Mwenge mpaka Ubungo (SAM NUJOMA),

Inahusisha ujenzi wa Barabara (13.5km), Vituo vya mabasi 20, Vituo vikuu vya mabasi (terminals) 2, Vituo vya mlisho (feeder stations) 10 na upanuzi wa daraja moja la Selander.

Lot 2: Kutoka Mwenge hadi Tegeta kupitia Barabara ya Bagamoyo. Inahusisha ujenzi wa Barabara (15.63km), Vituo vya mabasi 19, Vituo vikuu vya mabasi (terminals) 3, Vituo vya mlisho (feeder stations) 5, Madaraja manne kwenye barabara ya New Bagamoyo.

Lot 3: Karakana (Depot) 2 – moja eneo la Mbuyuni nyingine eneo la SIMU 2000, Kituo Kikuu (Terminal) ndani ya eneo la Kivukoni.

MIKATABA YA UJENZI NA USIMAMIZI– AWAMU YA NNE

LOT 1: KAZI ZA BARABARA

Mkandarasi wa ujenzi wa Lot 1 ni Kampuni ya China Geo-Engineering Corporation kutoka China; Mkataba ulisainiwa tarehe 30 Juni 2023; na muda wa ujenzi ni miezi 18. Gharama ya ujenzi ni Shilingi 174,380,157,323.00

LOT 2: KAZI ZA BARABARA

Mkandarasi wa ujenzi wa Lot 2 ni Kampuni ya Shandong Luqiao Group Co., Ltd kutoka China; Mkataba ulisainiwa tarehe 30 Juni 2023; na muda wa ujenzi ni miezi 18. Gharama ya ujenzi ni Shilingi 193,855,936,443.00

LOT 3: KAZI ZA MAJENGO

Mkandarasi wa ujenzi wa Lot 3 ni China Communications Construction Company Ltd kutoka China; Mkataba ulisainiwa tarehe 30 Juni 2023; na muda wa ujenzi ni miezi 18. Gharama ya ujenzi ni Shilingi 60,984,151,987.18
IMG-20250115-WA0015.jpg
IMG-20250115-WA0025.jpg
IMG-20250115-WA0059.jpg
IMG-20250115-WA0053.jpg
IMG-20250115-WA0047.jpg
IMG-20250115-WA0033.jpg

Soma: Interchange ya MWENGE na MOROCCO imepotelea wapi?
 
Back
Top Bottom